Yanga imefuta historia mbaya kwa Azam iliyodumu tangu 2014
Tangu mwaka 2014, Yanga ilikuwa haijapata ushindi dhidi ya Azam. Katika kipindi hicho, timu hizo zilikutana mara sita (6) kabla ya leo huku kichezo mitano timu hizo zikiwa zimetoka sare na Azam wakashinda mechi moja.
Yanga imepata ushindi ikiwa inakumbuka kipigo cha goli 4-0 walichokipata toka kwa Azam kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2017 ambacho kilikuwa ni maarufu kwa jina la 4G.
Goli pekee la Yanga kwenye mechi ya leo limefungwa na Obrey Chirwa Erasto Nyoni na golikipa Aishi Manula kutegeana kuwahi pasi iliyopigwa na Niyonima, Chirwa aliunasa mpira na kumtoka beki wa kati Yakubu Mohamed kisha kuachia shuti kali lililomshinda golikipa na kuzama kambani.
Ushindi wa leo unarudisha matumaini ya Yanga kutetea ubingwa wao baada ya kuejea kileleni kufatia kujizolea pointi tatu na kufikisha pointi 56 pointi moja mbele ya wapinzani wao Simba ambao kesho watakuwa na kibarua cha kuwakabili Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Mechi ya leo imeshuhudiwaikiongeza idadi ya majeruhi kwenye vikosi cha timu zote mbili. Yanga walipata pigo kwa kuondokewa na kiungo wao Justine Zulu ambaye alitolewa uwanjani kwa msaada wa machela na kuwahishwa zahati ya uwanjani kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kwa upande wao Azam, walimkosa mshambuliaji wao Yahaya Mohamed ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia. Yahaya alisababisha mpira kusimama mara kadhaa ili atibiwe lakini baadae alishindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutoka.
Post a Comment