TRA yatangaza kukusanya Tsh 10.87 trilioni kuanzia June 2016 mpaka March 2017

Mamlaka
ya Mapato Tanzania imekusanya kodi ya jumla ya Sh. Trilioni 10.87
katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2016/17 ambapo makusanyo
hayo ni sawa na ukuaji wa makusanyo ya asilimia 9.99
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi, Richard Kayombo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Mamlaka ya
Mapato Tanzania inawashukuru walipakodi wote ambao wameitikia wito.
“TRA
inatoa wito kwa kila mlipakodi kuwajibika kulipa kwa wakati pamoja na
kufichua wale wasiotimiza wao kikamilifu,”amesema Kayombo.
Aidha,
pamoja na mafanikio hayo kwa kipindi cha miezi tisa Mamlaka hiyo
itaelekeza juhudi zake katika kukusanya kodi mbali mbali ili kuhakikisha
lengo la mwaka la kukusanya Trilioni 15.1 linafikiwa.
Hata
hivyo, amesema kuwa TRA inazidi kusisitiza matumizi mashine za EFD
pamoja na zoezi la uhakiki wa TIN katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,
Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani linaendelea hivyo wananchi
wanatakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za EFD.
Post a Comment