MC ALGER WATUA DAR TAYARI KUIVAA YANGA JUMAMOSI
MC
Alger ya Algeria wamewasili nchini salama usiku huu, tayari kwa mechi
yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, Jumamosi.
MC
Alger wametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) na kupokelewa na baadhi ya maofisa wa ubalozi wao nchini.
Yanga
watakuwa wenyeji wa waarabu hao Jumamosi na imeelezwa wataweka kambi
kwenye Baraza la Maaskofu eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha MC Alger kimetua jijini Dar es Salaam na wachezaji wake wakionekana kujiamini tayari kwa mechi hiyo.
Post a Comment