DAKTARI YANGA AMPA RUHUSA NGOMA KUWAVAA WAARABU WA ALGERIA PALE TAIFA
Baada
ya kuwa nje ya uwanja kwa takriban mwezi mzima, straika wa Yanga,
Mzimbabwe, Donald Ngoma, amerejea kwenye kikosi hicho na yupo fiti
kucheza mbele ya Waarabu MC Alger ya Algeria kwenye mechi ya Kombe la
Afrika.

Ngoma
amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara tangu ulipoanza
mzunguko wa lala salama wa Ligi Kuu Bara, kiasi cha kumfanya ashindwe
kuitumikia Yanga kwenye michezo muhimu mbalimbali iliyokuwa mbele yao
ukiwemo ule dhidi ya Simba ambao walifungwa mabao 2-1.
Daktari
wa Yanga, Edward Bavu, alisema Ngoma ana asilimia 100 za kucheza mchezo
huo kwani yuko fiti na kwamba ana zaidi ya wiki mbili tangu apone
ambapo alikuwa akifanya mazoezi na timu.
“Sina
shaka tena na hali ya Ngoma ambaye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya
mguu, tayari amesharejea uwanjani na kwamba ana uhakika wa kucheza dhidi
ya MC Alger Jumamosi (kesho), hali yake kwa jumla inaridhisha sana na
kwamba amepata muda mrefu wa kufanya mazoezi na wenzake.
“Mashaka
yapo kwa Amissi Tambwe, kwani yeye alianza mazoezi jana (juzi), hivyo
siwezi kumpa asilimia nyingi za utimamu wa mwili wake kwani mazoezi yake
hayakidhi sana, hivyo kucheza kwake itategemeana na mahitaji ya mwalimu
na namna yeye atakavyomuona kwenye mazoezi haya ya siku mbili
zilizosalia.
“Ukiachana na hao, kuna Thabani Kamusoko na Justine Zulu, hawa hali zao bado haziko vizuri kwani hata mazoezi hawajaanza na Kamusoko aliumia siku moja kabla ya mchezo wetu na Azam, huku Zulu yeye akishonwa nyuzi sita baada ya kuumia kwenye mchezo huo,” alisema Bavu.
Post a Comment