Kampuni 9 za simu zilizopigwa faini na TCRA
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya TZS milioni 65
kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo
vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya 9,10 na 11 ya kanuni
za ubora wa huduma za 2011
Akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James
Kilaba amezitaja kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart,
Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited (Zantel), Mic
Tanzania Limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania
Telecommunications Company Limited (TTCL) huku akizitaka kampuni hizo
kuhakikisha zinatoa huduma bora.
Aidha
Mhandisi huyo amesema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa
kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo agizwa.

Post a Comment