KAGERA WAMENUNIA KURUDISHA POINTI TATU, WATUMA JOPO DAR
Kagera Sugar wameamua kufunga safari na jopo la watu watatu kwenda jijini Dar es Salaam.
Kinachowpeleka ni kile kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kitakachofanyika keshokutwa Jumanne.
Kagera inataka irudishiwe pointi zao
tatu baada ya Simba kushinda rufaa iliyobaini wao walimchezesha mchezaji
Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.
Mratibu wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein ndiye ataondoka jopo la Kagera jijini Dar.
Post a Comment