Bifu la Shigongo na WCB, Sallam Aibuka, Amwita Shigongo Mtabiri, Amuomba Atabiri Kama Serengeti Boys Watwaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya Vijana
Baada ya Bab Tale kumchana Mtunzi wa vitabu nchini Eric Shigongo kwa kuandika makala kupitia ukurasa wake wa Facebook akielezea watu watatu wanaompelekea Diamond Platnumz shimoni ambapo ndani yake aliwataja Bab Tale na Sallam, Meneja mwingine wa staa huyo aitwaye Sallam ameibuka na yeye kutoa ya moyoni huku akimwita mtunzi huyo mtabiri na kutaka ajaribu kutabiri kama timu ya vijana ya Serengeti Boys itaweza kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya Vijana yatakayofanyika chini Gabon kuanzia mwezi Mei.
Soma jinsi Bab Tale Alivyomchana Shigongo HAPA
Soma jinsi Bab Tale Alivyomchana Shigongo HAPA
Mbali na hilo, Sallam ameweka ratiba ya shoo za Diamond Platnumz atakazozifanya mwaka huu huku pia akiweka shoo alizozifanya staa huyo mwaka jana.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Sallam ameandika hivi;
"Baada ya kuona post ya yule jamaa mtunzi wa Vitabu ambae sasa ameamua kuchukua kazi ya Utabiri, najua yupo kwenye Kamati ya Serengeti Boys naomba ututabirie matokeo kabisa kama tunachukua Kombe au La!
"Diamond ana show Leaders Club Tarehe 22 July 2017, halafu ana show zaidi ya 10 kwenye mikoa tofauti nchini mwezi wa Nov-Dec
"Mwaka Jana Show za Diamond alizofanya Tanzania
1.Mabibo Hostel Kiingilio Bure
2.U-DOM Dodoma Kiingilio Bure
3.CCM Kirumba Mwanza
4.Wasafi Beach Party Dar.
5.Wasafi Festival Iringa.
"Unachotakiwa kulalamika kuwa kwanini hafanyi Show Dar Live, hapo tungeelewana hata na mie ningekusapoti." Amemaliza kuandika Salaam
Kwa jinsi hali inavyoonekana kuna jambo ambalo haliko sawa kati ya watu hawa wanne Shigongo, Sallam, Bab Tale na Diamond ndiyo maana jana mameneja hao wa WCB wamepost bango linaloonyesha kuwa WCB watakuwa na shoo Escape One katika sikukuu ya Pasaka huku naye Diamond akipost bango hilo na kuondoa bango la awali aliloliweka juzi lililokuwa linaonyesha WCB kuwa watapiga shoo Dar Live wakati wa sikukuu hiyo ya Pasaka.
Kujua mjadala huu ulipoanzia bonyeza hapa: WATU WATATU WANAOMPELEKA DIAMOND SHIMONI
Kujua sehemu ya pili ya makala ya Shigongo na alivyojibu Bab Tale bofya hapa: SAKATA LA DIAMOND NA SHIGONGO LACHUKUA SURA MPYAKujua mjadala huu ulipoanzia bonyeza hapa: WATU WATATU WANAOMPELEKA DIAMOND SHIMONI
Soma sehemu ya mwisho ya makala ya shigongo hapa: SHIGONGO AMALIZA MJADALA WAKE NA DIAMOND
Post a Comment