Askofu Gwajima Kununua Treni ya Umeme
Mchungaji
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria
kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya
kujenga reli ya kisasa(standard gauge).
Amesema
kuwa treni hiyo itatumika siku za ibada kubeba waumini huku wakiimba
nyimbo za kumtukuza Mungu. Lakini pia alisema atakuwa tayari kuruhusu
itumike kubeba abiria wa kawaida.
Askofu
Gwajima aliyasema hayo jana kanisani kwake, ambapo alieleza gharama za
treni hiyo ni TZS bilioni 11 lakini hakusema ni lini hasa atainunua.
“Siku
moja nilimchukua mwalimu Bihagaze, alikuwa mwalimu wangu wa Biblia,
nikamwambia twende nikakuonyeshe mji wa mwanakondoo, nikamchukua na
helkopta hadi shambani ambapo ni mji utakuwa na mahoteli, universities,
kituo cha mafuta na kila kitu,” alisema.
Alifafanua kuwa katika mji huo, kuna ramani inaonyesha kuwa reli inapita katikati. “Alipopaona
akasema mbona kuna reli inapita katikati, nikamwambia nitanunua treni,
akashangaa akaniuliza, treni ni shilingi ngapi? Nikamwambia dola milioni
nne na mabehewa yake dola milioni tano hivi, akasema nikulipie?
Nikamwambia nitanunua mwenyewe. Akapiga magoti kusujudu nikamwambia yapo
mengi yanakuja,” alisema Askofu Gwajima huku waumini wake wakimshangilia kwa shangwe.
Ujenzi
wa reli uliozinduliwa na Rais Dkt Magufuli Aprili 12 mwaka huu,
utakamilika ndani ya miezi 30, ambapo kwa awamu ya kwanza utaanzia Dar
es Salaam hadi Morogoro, treni ikiwa na uwezo wa kukimbia umbali wa
160km/hr. Treni itakuwa na jumla ya mabehewa 100.
Post a Comment