WENGER AUOMBA UONGOZI WA ARSENAL AONGEZEWE MIAKA MIWILI
Kocha Arsene Wenger ameauambia uongozi wa Arsenal kwamba anataka kuendelea kubaki Emirates kwa miaka miwili.
Katika mkutano pamoja
na uongozi wiki iliyopita, Wenger ameweka wazi yake ya moyoni kuwa
angependa kubaki kwa miaka miwili zaidi ili afanye mabadilike.
Kwa mujibu vya vyanzo,
kwamba Wenger ameona makosa yalipo na anataka kubadilisha ndiyo maana
anaomba miaka hiyo miwili ingawa haijaelezwa kuwa baada ya hapo
ataondoka au ataendelea kubaki.
Hata hivyo, Wenger anaweza kuwa na wakati mzuri wa kupata mkataba mpya kama Arsenal itaitwanga Man City wikiendi hii.
Kama atafungwa atakuwa ameingia kwenye hofu mpya na huenda uongozi wa Arsenal unaweza kuamua tofauti.
Post a Comment