Waziri Mkuu Kaagiza viongozi wa 'WETCU' Wakamatwe Haraka
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora
kuwakamata viongozi wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU)
pamoja na kufunga ofisi za chama hicho kupisha uchunguzi wa tuhuma za
ubadhirifu.
Pia
Waziri Mkuu amevunja Bodi ya WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania
- TTB kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi
mabaya ya fedha za umma.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo leo jioni katika kikao kilichofanyika kwenye
ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora, ambapo amesema Mheshimiwa
Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Bw. Vita
Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Bw. Wilfred Mushi.
Viongozi
wa WETCU ambao Waziri Mkuu ameagiza wakamatwe ni Mwenyekiti Bw.
Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa
Ndani na Mhasibu Mkuu. Pia amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha
uhasibu wa chama hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.
“Kuanzia
sasa watumishi wote wa kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti
nimewasimamisha kazi pamoja na Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius
Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo
timu ya ukaguzi itakapokamilisha kazi yake,” amesisitiza.
Waziri
Mkuu amesema kwa muda mrefu wakulima wameteseka na zao hilo kukosa tija
kwa sababu ya usimamizi mbovu wa viongozi wa ushirika na Bodi ya
Tumbaku Tanzania jambo ambalo Serikali haiwezi kulivumilia.
Amesema
“Hatuwezi kuwa na ushirika ambao hauwasaidii wanachama. WETCU walipokea
sh. bilioni 15 ambazo walizikatia risiti na hazijaonekana. Pia
waliwalipa wazabuni sh, bilioni 10 ambazo hawajazikatia risiti,”.
“Wakati
wanachama ambao ni wakulima wakiendelea kutesema WETCU walinunua gari
la sh. milioni 269 kinyume na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa wadau ambao
ulipitisha zitumike Shilingi milioni 40 tu,” amesema.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa chama hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji
kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo
limechangia wakulima wa tumbaku kukosa tija.
Amesema
WETCU kimekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha ambapo alitolea mfano
suala la ukarabati wa ofisi tatu ikiwemo ya makao makuu ambayo ilipangwa
ikarabatiwe kwa sh. milioni 33 wakatumia sh. milioni 170 na ofisi za
Tabora na Urambo zilipangiwa sh. milioni tano kila moja na
hazikukarabatiwa.
Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi wakati ikiwa inazalishwa hapa nchini.
Aidha,
alimepiga marufuku matumizi ya kwa dola katika sekta ya tumbaku na
badala yake zitumike fedha ya Kitanzania kwa sababu kitendo hicho
kimekuwa kiwanyonya wakulima.
Post a Comment