Ukumbi mpya wa CCM wapewa jina la Kikwete
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wamekubaliana kuita ukumbi mpya uliopo eneo la Dodoma Makulu ‘Kikwete Hall’.
Makubaliano
hayo yametokana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Dk John Magufuli
kupendekeza kwa wajumbe hao ukumbi huo uitwe Kikwete.
“Leo
tumekaa katika ukumbi huu mzuri kuna watu wamefanya kazi na miongoni
mwao atakuwa ni Mzee wetu Jakaya Kikwete (Rais Mstaafu wa awamu ya nne).
Mtakumbuka kabla ya hapa tulikuwa tukikaa kule yanatolewa magunia
tunakaa,”amesema.
Wajumbe hao walikubaliana na wazo hilo na baadaye Rais Magufuli walishikana mkono na Rais Kikwete.
Post a Comment