Magufuli: Hatuna Muda wa Kumbembeleza Mtu Kukichangia Chama Chetu
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli amesema chama hicho hakitambembeleza mtu kukichangia katika shughuli mbalimbali.
Akihutubia
mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika leo Dodoma, Dk Magufuli amewaambia
wajumbe wa mkutano huo kuwa kwa miaka yote CCM kimekuwa kikiomba hata
kwa watu ambao hawastahili.
“Matokeo
yake wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kudhalilisha. Hakuna tena omba omba
hatutaki kumbembeleza mtu akitaka kutuchangia atuchangie,”amesema.
Amesema
kuwa chama hicho kina utajiri unaokiwezesha kujitegemea na kwamba
mwanachama atakayetumia mali za chama kwa maslahi binafsi atachukuliwa
hatua kali.
Post a Comment