TANZIA:MSANII SNURA AFIWA NA MNENGUAJI WAKE
Msanii wa muziki Snura Mushi amepata majanga baada ya kufiwa na mnenguaji wake aliyefahamika kwa jina la Faidha.
Marehemu
anadaiwa kufariki dunia hivi karibuni ikiwa ni siku chache baada ya
kujifungua huku chanzo cha kifo chake kikiwa hakijafahamika.
Snura amedai Faidha ameondoka wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika lakini hana la kufanya zaidi ya kumshukuru Mungu.
“Dah!
nimeumia sana, siwezi kusimulia msiba wa Faidha kwani umenishitua sana,
wanaomjua wanaelewa alivyokuwa akinipa sapoti kwenye shoo zangu ila
hatuna la kufanya zaidi ya kumuombea kwa Mungu,” Snura aliandika
Istagram.
Aliongeza,
“Nimebaki na picha zako tu mwenyewe haupo, pacha wangu mamaangu mdogo
wangu Faidha wangu umeniweza, Faidha umeniweza naumia jamani naumia
mwenzenu Faidha ni kweli sikuoni tena siongei na wewe tena hata kwenye
simu jamani Faidha wangu kaenda kaenda Faidha,”
Post a Comment