RATIBA KAMILI YA MAANDALIZI YA SERENGETI BOYS HII HAPA
Wakati
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likirejesha nyuma kwa wiki
moja, timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17
maarufu kwa jina la Serengeti Boys inatarajiwa kuanza kambi mpya Machi
12, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Serengeti
Boys itakuwa kambini Dar es Salaam hadi Machi 26, mwaka huu ambako
itakwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mechi za kirafiki za
kimataifa kujiandaa na michuano Afrika ambayo sasa itaanza Mei 14, 2017
badala ya Mei 21, mwaka huu.
Michezo
ya kirafiki ya kimataifa itakuwa ni dhidi ya timu za vijana za Rwanda
(Machi 28, 2017), Burundi (Machi 30, mwaka huu) na Uganda Aprili 2,
mwaka huu). Michezo yote itafanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani
Kagera.
Sababu
za kuwa na mechi hizo Bukoba ni kupunguza gharama kwa TFF kwani ni
rahisi kusafirisha timu hizo kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi na
Uganda.
Timu
hiyo itarejea tena Dar es Salaam Aprili 3, mwaka huu ambako siku
inayofuata itaagwa kwa kupewa bendera na mmoja wa viongozi wa nchi kabla
ya kusafiri Aprili 5, mwaka huu kwenda Morocco kwa ajili ya kambi.
Timu
hiyo itaunganisha kwenda Cameroon Mei mosi, mwaka huu ambako Mei 3,
2017 itacheza mechi ya kwanza na Cameroon kabla ya kurudiana Mei 6,
mwaka huu na siku inayofuata itakwenda Gabon.
Serengeti
Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo
imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola.
Ina lalengo ya kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
La
ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa
mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali za
Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu.

Post a Comment