Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. Magufuli Aendesha Kikao Cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Ya Taifa Ya CCM Jijini Dar Es Salaam
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akijiandaa kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama
cha Mapinduzi CCM leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM
(Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa
kikao hicho jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana
na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt.
Ali Mohamed Shein mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi CCM Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa kikao
cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM
kilichofanyika jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Post a Comment