Inasikitisha, Dereva Bodaboda Aliyegongwa na Range Rover ya Jaguar, Kumbe Aliacha Barua Nzito, Isome Hapa
GARI ya kifahari aina ya Range Rover yenye namba za usajili KCB 808J inayomilikiwa na staa wa muziki nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi maarufu kwa jina la Jaguar iligonga na kuua vijana wawili waliokuwa kwenye bodaboda katika njia panda ya Makutano-Sagana Machi 22 mwaka huu.
Range Rover ya Jaguar ikiwa eneo la ajali. |
Vijana hao wawili waliopoteza maisha papo hapo walitambulika kwa majina ya Joseph Maingi na Sinforan Mugo Mwangi.
Familia ya Sinforan Mugo Mwangi imetoa barua iliyoandikwa na marehemu Februari 27, 2017 kabla ya kifo chake ikielezea alivyokuwa mtu wa kuishika dini na maombi yake kwa Mungu.
Jaguar alipokwenda kuifariji familia ya marehemu Mugo. |
Katika barua hiyo, Marehemu alikuwa anamuomba Mungu amsamehe dhambi zake pamoja na kumuomba amjalie apate kiasi cha shilingi 200,000/= za Kenya zaidi ya shilingi 4,000,000/= za Tanzania ili aweze kujenga nyumba na kununua pikipiki. Mugo aliahidi kutoka fungu la kumi kwa kiasi ambacho angekipata kama shukrani kwa Mungu baada ya kujibu maombi yake.
Barua aliyoiacha marehemu Mugo. |
“Ninakuja mbele zako nikiomba msamaha maana nimetenda dhambi Bwana, ninaomba msamaha wako Bwana maana wewe ndiye mwenye uwezo wa kutoa msamaha kupitia jina la mwanao wa pekee Yesu Kristu. Nisamehe dhambi zangu.
“Bwana Mungu wangu ninaomba unisaidie nipate kiasi cha Ksh 200,000/= ili niweze kujenga nyumba na ninunue pikipiki pia naomba unikumbushe kutoa fungu la kumi pamoja na sadaka mara baada ya kufanikiwa kupata fedha hizo. Mungu wangu, ninaomba uwepo wako katika maisha yangu na niweze kukupenda wewe kila wakati maana wewe ni baba mwenye upendo," aliandika Mugo
Post a Comment