ad

ad

MUIGIZAJI LEE NELSON AVAMIA NDEGE YA WACHEZAJI ENGLAND, POLISI WAMSHITUKIA



 Mchekeshaji mahiri nchini England, Lee Nelson ameendeleza vituko vyake baada ya kuingilia safari ya timu ya taifa ya England.
Timu hiyo ya taifa ya soka ilikuwa inaondoka kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kambi kabla ya kwenda Brazil kwenye
 Kombe la Dunia.

Nelson akazuga naye ni kati ya wachezaji, akawa bize 
kinoma kabla ya kushitukiwa.
Steven Gerrard ndiye alianza kushitukia kuhusiana na 
mchekeshaji huyo.
Polisi wakaitwa na kumkokota Nelson, wakamtoa
 kando huku akiwa amevaa suti zinazoringana na 
wachezaji wa England kabisaa utadhani naye ni mhusika.
Wakati Fulani aliwahi kuvamia mazoezi ya Man City 
lakini kipa Joe Hart akamshitukia.


GERRARD AKIMSHANGAA


AKITOLEWA
Picha za chini zinaonyesha alivyowahi kuvamia mazoezi ya Man City kabla ya kushitukiwa na kutolewa.

No comments

Powered by Blogger.