ad

ad

Wema Afikishwa Kortini Kisutu, Aachiwa Kwa Dhamana


Wema Sepetu na wafanya kazi wake wakipandishw akwenye karandiga la polisi kuelekea mahakamani.
DA RE SALAAM: Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu na wafanya kazi wake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na akusomewa mashtaka matatu ambayo yote yanahusiana na matumizi ya bangi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wema na wenzake hao wamekana mashtaka hayo na kuruhusiwa kupewa dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja pamoja sambamba na kuwa na wadhamini wawili kila mtuhumiwa.
Kesi hiyo inaendeshwa na Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ambapo mawaakili kwa upande wa watuhumiwa ni Alberto Msando na upande wa serikali ni Pamela Shinyambara pamoja na Nassoro Katuga.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 28 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.Wema na wenzake wakishuka mahakamani Kisutu
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro jana alesema kuwa jeshi lake bado linamshikilia Wema na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo na kuwa jalada lao limepelekwa kwa wakili wa serikali alipitie ili aone ushahidi uliopo pamoja na kupata majibu kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kubaini kama kweli ni mtuamiji wa madawa ya kulevya na baada ya hapo atafikishwa mahakamani.

No comments

Powered by Blogger.