Vita ya dawa za kulevya: Watuhumiwa 12 kati ya 112 Wapandishwa Mahakamani akiwemo Wema Sepetu
Sakata
la Madawa ya kulevya limeendelea kugonga vichwa vya habari wiki hii
ambapo Jumatatu hii Jeshi la polisi limedai toka lianze operesheni hiyo
tayari limewakamata watuhumiwa 112 na kati ya hao 12 wamepandishwa
mahakamani Jumatatu hii kwajili ya kiapo cha kutorudia matumizi ya
Madawa ya kulevya baada ya kukiri kutumia.
Kati ya watu hao 12 ni pamoja na Wema Sepetu, Romy Jones, Petit Man, TID pamoja na wengine.
Aidha
Wema Sepetu baada ya kiapo hicho atarudishwa polisi kwajili ya
kuandaliwa shtaka jipya linalomkabili la kukutwa na msokoto wa bangi
nyumbani kwake.
Akiongea
na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar
es Salaam, Simon Sirro amesema watuhumiwa wengi waliohojiwa walikiri
kutumia Madawa ya kulevya na kati ya hao walieleza watu ambao
wanawauzia.
“Tumewakamata
watuhumiwa jumla 112 na tumekamata kete 299 zinazodhaniwa ni za Madawa
ya kulevya na kwa kawaida haya Madawa Mkemia Mkuu wa serikali yeye ndiye
atakayetuambia ni Madawa ya aina gani,” alisema Kamanda.
Aliongeza, “Katika
watuhumiwa 112, kuna watuhumiwa 12 tumewapeleka leo mahakamani,
tumewapeleka mahakamani kwa sababu sheria ya mwenendo wa mashtaka iko
wazi kifungu cha 73 na 74, huwa tunaweza kuomba kwa mweshimiwa hakimu
kuwaombea watuhumiwa kwa kiapo, kwamba hawa watuhumiwa tunataka
wabadilishe tabia zao. Tunawapeleka mahakamani ili wakae chini ya
uangalizi wa jeshi la polisi na mahakama kwa muda wa miaka 2 wasifanye
makosa tena,”
“Kwa
sababu tulichokibaini kwa wote tuliowakamata wengine wanakiri na
wamekwenda kuonyesha hayo Madawa ya kulevya. Kwa hiyo kusudio la kwanza
wawe chini ya uangalizi wetu, na kusudio la pili la kiapo chetu waache
hiyo tabia ili wabadilike wawe raia wema, lakini la tatu tumeomba wale
wanakuja kuripoti kituoni angalau mara mbili kwa mwezi na lengo letu ni
kuona hawa ndugu zetu ambao walikuwa wanavuta madawa ya kulevya wamecha
kabisa,”
Post a Comment