Ester Bulaya Apinga Kitendo cha Kuwakamata Waathirika wa Madawa ya Kulevya na Kuwatupa Selo
Mbunge
wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya amefunguka na kutaka siasa isiingizwe
kwenye vita ya madawa ya kulevya na kusema viongozi wasimdanganye Rais
Magufuli ili kujihakikishia vyeo vyao au nafasi zao katika uongozi.
Ester
Bulaya ametoa rai hiyo leo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa
taarifa za kamati na kusema Rais anapaswa kuambiwa ukweli ili waweze
kumsaidia kupambambana vyema na madawa ya kulevya.
"Tusifanye
siasa kwenye vita hii ya madawa ya kulevya, tusimuongopee Rais kwa
kutaka kuhakikisha vyeo vyetu tumwambie ukweli, ili kumsaidia Rais
anapaswa kumteua kamishina wa hii tume maana tangu tulipopitisha sheria
hiki chombo hakina kamishna, tutakapo hakikisha hicho chombo kinapata
kamishna kwa kumsaidia Mhe. Rais tutakamata wale wanaoingiza dawa za
kulevya wale mapapa na si hao wanaokamatwa sasa hivi" alisema Bulaya
Mbali
na hilo Mbunge Ester Bulaya amesema kuwa hawa watu wanaokamatwa saizi
wanapaswa kupelekwa mahospitali kupata matibabu na si vinginevyo kwani
hao ni waathirika wa dawa.
Post a Comment