ad

ad

SIMBA SC YATWAA KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR


Mshambuliaji wa timu ya Simba Emanuel Okwi, akimpita beki wa timu ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa fainali ya Kombre la Mapinduzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


KLABU ya Simba imetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa penalti 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya matokeo ya 0-0 katika dakika 90, usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Penalti za mabingwa hao mara tatu wa Kombe la Mapinduzi ziliwekwa kimiani na Awadh Juma, Hassan Kessy 'Danny Alves', Hassan Isihaka na Dan Sserunkuma huku za Mtibwa Sugar zikifungwa na Ally Lundenga, Shabaan Nditi na Ramadhan Kichuya.
Katika michuano hiyo, Simon Msuva wa Yanga ameibuka mfungaji bora akiwa na mabao 4, Salim Mbonde wa Mtibwa akichukua tuzo ya mchezaji bora huku kipa wa Mtibwa, Said Mohammed akiwa ndiye kipa bora wa michuano hiyo iliyomalizika usiku huu.
Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa akimpita beki wa timu ya Simba katika mchezo wa fainali ya Kombev la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar usiku huu.








Wachezaji wa Timu Simba wakishangilia Ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi baada ya kushinda Mchezo wa Fainali na Timu ya Mtibwa kwa kuifunga 4--3

No comments

Powered by Blogger.