MANJI AENDELEA KUSOTA CHINI YA ULINZI, AHOJIWA TENA UHAMIAJI
Huku
kikosi cha Yanga kikishuka dimbani leo kuivaa Simba, Mwenyekiti wake,
Yusuf Manji jana alikuwa akihojiwa na Jeshi la Uhamiaji kuhusu tuhuma za
kuwa na hati za kusafiria za nchi mbili.
Habari
zinasema kwamba, Manji jana alitumia karibu kutwa nzima katika ofisi za
Uhamiaji akihojiwa na hakukuwa na taarifa yoyote ile kuhusu kufikishwa
mahakamani au vinginevyo. Hadi saa 9:00 alasiri chanzo chetu kilidai
Manji alikuwa bado anahojiwa. Hii ni mara ya pili anahojiwa ndani ya
wiki moja.
Mmoja
wa watu wa karibu wa Manji amesema kuwa, Manji jana alianza kuhojiwa na
Uhamiaji asubuhi halafu kukawepo na taarifa taarifa za kufikishwa
mahakamani lakini Uhamiaji haikutoa taarifa yoyote kuhusu suala hilo
hadi jana usiku.
“Manji
amepelekwa Uhamiaji kwa mahojiano labda akitoka huko ndipo anaweza
kwenda mahakamani, lakini Uhamiaji hawajatueleza jambo lolote lile,”
alisema.
Baada ya gazeti hili kusubiri kwa muda mrefu kujua hatima ya Manji, tulipokitafuta tena chanzo chetu kilisema;
“Bado
anahojiwa na Uhamiaji na hatujui nini kitatokea lakini leo na
ataendelea kuwa chini ya ulinzi kwani atarudi tena hospitalini.”
Hii
ina maana Manji atabaki Hospitali ya Aga Khan chini ya uangalizi wa
Uhamiaji hivyo leo hatokuwepo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuishuhudia
Yanga ikicheza dhidi ya Simba katika Ligi Kuu Bara.
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment