ETI YANGA IIFUNGE SIMBA, SOMA MANENO YA JAMHURI KIWHELO JULIO
Kocha
 wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema Yanga haina jeuri 
ya kuifunga timu yake hiyo ya zamani katika mchezo wao wa leo Jumamosi 
kwani Wekundu wa Msimbazi wana kikosi imara.
Julio
 amesema huko nyuma Yanga iliinyanyasa Simba kwa kuwa haikuwa na kikosi 
imara kama ilivyo sasa, hivyo leo ushindi kwao ni jambo la kawaida.
Simba
 inaongoza ligi ikiwa na pointi  51 katika mechi 22 ikifuatiwa na Yanga 
yenye pointi 49 katika michezo 21. Timu hizo zinakutana leo Jumamosi 
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza
 na Julio alisema kuwa, Simba ni lazima ishinde ili kudhihirisha uwezo 
wa timu yao na dhamira ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.
 “Simba
 lazima wawe mabingwa msimu huu kuhakikisha tunashinda Jumamosi (leo), 
timu inacheza vizuri na wachezaji wanacheza kitimu  hivyo Yanga wasahau 
suala la kutwaa ubingwa msimu huu. “Kuhusu ligi ya safari hii haina 
ushindani mkubwa kwani timu hazina fedha za kutosha kwani zile za 
wadhamini hazijitoshelezi hivyo kusababisha timu nyingine kushindwa 
kufanya vizuri,” alisema Julio.
“Ni
 Simba na Yanga labda na Azam ndizo zinazoonyesha upinzani wa haki 
lakini hizo nyingine zilizobaki ni kama zinajikongoja tu kwani hazina 
uwezo wa kupambana na vigogo hao."
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment