BARCELONA WAKABIDHIWA 'LAINI' YA 4G NA PSG, DI MARIA ATUPIA MBILI
PSG
imeonyesha inaweza baada ya kuitwanga Barcelona kwa mabao 4-0 katika
mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya.
Barcelona
ikiwa ugenini jijini Paris imeshindwa kuonyesha cheche licha ya
kuongozwa na nyota wake Lionel Messi na Neymar na kujikuta ikipokea
kipigo hicho cha kondoo mchovu.
Angelo
Di Maria ametumbukia nyavuni mara mbili huku Endson Cavani aliyetimiza
miaka 30 jana akifunga moja na Julian Draxler akifunga moja.
Mechi nyingine Benfica imeifunga Borussia Dortmund kwa bao 1-0.
Post a Comment