Wema aweka rekodi ya ajabu!
DAR ES SALAAM: STAA wa filamu ‘grade one’ na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu
ameweka rekodi ya ajabu ya kuwa staa wa kwanza nchini kutumia magari
mengi ya kifahari ndani ya kipindi cha miaka kumi mfululizo, Ijumaa
linakuchambulia.
Katika chimbachimba iliofanywa na Ijumaa
imebaini kuwa, mlimbwende huyo mwenye mvuto katika vyombo vya habari
hadi sasa ameshateketeza mamilioni ya shilingi kwa kutembelea magari
yenye thamani kubwa, huku kwa sasa ikidaiwa hana usafiri wa kueleweka.
Toyota Lexus (mil. 40)
Mwaka 2012 aliuanza vema baada ya
kudaiwa kununuliwa gari hilo na kigogo mmoja (jina linahifadhiwa) lenye
thamani ya shilingi milioni 35 (sokoni milioni 28 hadi 35).
Hata hivyo gari hilo hakukaa nalo sana kwani baada ya kupata lingine (Toyota Mark X) aliamua kumpatia mama yake kama zawadi.
Toyota Mark X (mil.35)
Baada ya kuachana na Lexus, alivuta gari
jipya (Mark X) ambalo alidai lilikuwa na thamani ya shilingi milioni 38
(kwa sasa sokoni ni milioni 28 hadi 35).
Katika gari hilo, Wema alidai ameamua kufikia uamuzi wa kulinunua ili kubadilisha mazingira.
Audi Q7 (mil. 80)
Alianza kuonekana nalo kwa mara ya
kwanza mwaka 2013 katika Fukwe za Coco jijini Dar ambapo aliweka picha
mtandaoni na kusema kuwa amepata ‘baby’ mpya ambaye yupo naye beach.
Hata hivyo ilikuja kujulikana baadaye
kuwa gari hilo alipewa na kigogo mmoja aliyekuwa akitoka naye kimapenzi
kipindi hicho (jina linahifadhiwa) ambalo alimnunulia kwa bei ya
shilingi milioni 80.
BMW 545i (mil. 45)
Alizawadiwa mwaka 2014 na meneja wake,
Martin Kadinda katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika
alikopanga zamani, Kijitonyama jijini Dar.
Gari hii lilikuja kuleta mkwaruzano
baada ya aliyekuwa bwana’ke, Diamond Platnumz kukataa kuwa Kadinda
hawezi kulinunua. Thamani yake ilitajwa kuwa ni milioni 56 wakati sokoni
linapatikana kwa milioni 40 hadi 45.
Nissan Murano (mil.36)
Siku hiyohiyo pia, aliyekuwa mpenzi wake
enzi hizo, Diamond alimkabidhi Wema gari hilo lenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 36.
Diamond ambaye alikuwa akitamba na Wimbo
wa Number One alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kumpongeza
siku yake ya kuzaliwa na kuweka wazi kuwa ameamua kumzawadia gari.
Range Rover Evogue (mil.140)
Ilikuwa mwaka 2015 katika kusherehekea
siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika Millenium Towers, Kijitonyama jijini
Dar. Katika usiku huo aliosindikizwa na mastaa kibao wa filamu Bongo,
Wema aliwatoa hadi nje ya ukumbi huo na kuwaonesha gari hilo ambalo
alidai amejizawadia (pichani juu).GAZETI LA IJUMAA
Baada ya kuwaonyesha, alitupa madongo
kwa Diamond ambaye alikuwa ameshaachana naye na kusema kuwa si wa
kuhongwa vigari vya dola elfu 30 (milioni 30).
Hata hivyo, alidai gari hilo lina thamani ya shilingi milioni 200 wakati sokoni linapatikana kwa bei ya shilingi milioni 140.
Atumia milioni 376
Ijumaa Wakati kukiwa na madai kuwa nyota huyo
asiyechuja hivi sasa hana ndinga, mahesabu yanaonyesha kuwa ukiondoa
gari alilozawadiwa kama mshindi wa Shindano la Miss Tanzania 2006, Wema
Sepetu ametumia zaidi ya shilingi milioni 376 kwa ajili ya magari peke
yake, rekodi ambayo inaweza kuwa haijawekwa na staa mwingine yeyote
Bongo.lilimtafuta Wema ili kujua kwa sasa anatumia gari gani lakini jitihada hazikuweza kuzaa matunda baada ya simu yake kutopatikana.
Paparazi wetu pia alijaribu kufika
nyumbani kwa Wema, maeneo ya Ununio nje kidogo ya Jiji la Dar na
kuambiwa kuwa, hayupo lakini ndani kulikuwa na gari ya silva ambayo
haikujulikana ni aina gani na kama ni yake au ya ndugu yake.
Jitihada za kujua kwa sasa staa huyo mkubwa anatumia usafiri gani zinaendelea.
CHANZO: GPL
CHANZO: GPL
Post a Comment