Chuchu: Mtoto Ameongeza Mahaba kwa ‘Baby’..!!!
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans ambaye hivi karibuni
alijifungua mtoto wa kiume (Jayden), amesema mtoto huyo ameboresha
mahaba niue kwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Chuchu alisema mtoto huyo amekuwa ni
faraja kwao wote na mapenzi yameongezeka baina yake na mpenzi wake huyo
kitu ambacho anamshukuru Mungu.
“Jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu, mahaba yamezidi asilimia ni jambo la
kumshukuru sana aliye juu maana bila yeye kusingekuwa na kitu kabisa na
ninamuomba atimize mambo mengine makubwa zaidi,” alisema Chuchu.
Post a Comment