Mchungaji kizimbani kwa tuhuma za kubaka mwanaye
Mchungaji
wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (FPCT) Tawi la Gezaulole
wilayani Hai, Emanueli Mwikizu (42) amefikishwa katika Mahakama ya
Wilaya ya Hai kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 7.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgD8RrslDWb0n7tTcJJlLu-dNL3yjn7qCa9dj6l60DWAFwp0rquHdW5199iuJrU9nNTMVy7nABphDMUm13e21qROPll4SRGEI8D8MOngRlfikjy9p3Z24QQAHMXeSDRJxFet1cE1wElPyA/s640/1.jpg)
Akisoma
hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza kesi
hiyo, Anold Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha Moleli
amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kuzini akijua kufanya hivyo ni
kosa la jinai.
Alisema
kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu
nyumbani kwake mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa
kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za
siri.
Mtuhumiwa
huyo alikana shtaka hilo ambapo hakimu anayesikiliza kesi hiyo
aliharisha hadi Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa yupo
rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.
Post a Comment