Kiba, Diamond Wamkacha Shehe Mkuu, Kujua ni wapi soma Hapa!
STORI:RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Ama kweli
imeshangaza wengi! Kitendo cha nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ na Ally Saleh Kiba kushindwa kutokeza kwenye sherehe za
kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaani Maulidi
iliyofanyika wilayani Temeke jijini hapa ambapo walialikwa na Shehe Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na kumuahidi kuwa
wangefika.
Katika Maulidi hiyo ambayo ilifanyika
Mtaa wa Liganga wilayani hapo na mwenyeji wa shughuli hiyo kuwa Shehe
Alhad, ilihudhuriwa na waheshimiwa mbalimbali wakiwemo Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania,
Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir na
wengineo.Shehe Mkuu wa Dar, Alhad Mussa Salum akiwa na waandishi na wahariri wa Global Publishers.
KAULI YA SHEHE MKUU JUKWANI
Wakati Maulidi hiyo ikiendelea, Shehe
Alhad aliutangazia umati uliojaa kuwa, katika hafla hiyo aliwaalika
wasanii mbalimbali na kuwataka watu kuwachukulia wasanii hao kama
wenzao. Akiendelea kuweka mambo sawa, alisema mpaka muda huo msanii
ambaye alishafika ni Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na pia akaongeza kuwa,
msanii wa nyimbo za kughani, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ alikuwa njiani kufika
eneo la tukio ingawa mpaka wageni waalikwa wanaondoka, Mpoto alikuwa
hajafika.
Baadhi ya watu walifurika kwenye eneo
hilo na kujua kuwa, Diamond na Kiba wangekuwepo, walishangaa kuona muda
unakwenda bila wapendwa hao kuonekana licha ya kusubiriwa kwa hamu
kubwa.
Diamond
KAMA WANGEFIKA
Baadhi yao walisema kuwa, kama Diamond
na Kiba wangejitokeza kwenye Maulidi hiyo, wanaamini Shehe Alhad
angewaunganisha na kuwashikanisha mikono ya wengine wakiwa hawezi hata
kuongea.
Uokoaji huo ulishuhudiwa na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja
Jenerali Ezekiel Kyuga ambao walishiriki bega kwa bega na waokoaji
tangu lilipotokea janga hilo. Kufuatia kufanikiwa kwa zoezi hilo,
mashuhuda walilipuka kwa shangwe na kuwapokea wachimbaji hao ambao kati
yao walikuwemo wenye uwezo wa kuongea ambao walisimulia tukio
lilivyokuwa pamoja na kusema kuwa ni kama walikuwa kuzimu na kwamba
walikuwa na hofu kwa muda wote wakiamini walikuwa wamesahaulika.Ali Kiba
Kabla ya kuokolewa, yalifanyika
mawasiliano ya kuwatumia ujumbe kwa kutumia waya ili waseme wako wangapi
na majina yao, ambapo walisema kuwa wako 15 na kwamba walikuwa na njaa
na walihitaji maji, soda na sigara. Akizungumza na Wikienda juu ya
chanzo cha tukio hilo, msemaji wa mgodi huo, Fracis Kiganga alisema kuwa
chanzo cha tukio hilo ni mazingira duni ambayo siyo salama kutokana na
uduni wa vifaa wanavyotumia mgodini humo.
Mbali na Mchina huyo, Meng Juping, wengine waliookolewa ni Ezekiel
Bujiku (20), Yohana Shigangama (34) na Aniset Masanja (32). Wengine ni
Dikson Moris (25), Mussa Cosmas (28), Raphael Nzubi (26), Amani
Silvester (26), Sheku Butogwa (22), Hassan Idd (31), Augustino Robert
(27), Mgalula Kayanda (23), Sabato Philimon (30) na mmoja ambaye jina
halikutambulika haraka.
upendo hali ambayo ingeweza kumaliza
bifu lao. “Jamani hawa jamaa zetu kina Diamond ndiyo kusema hawaji au
wameshaondoka? Nasikia nao walialikwa. Unajua ni kutokuwa na uelewa tu,
kama wangefika, lazima wangepatanishwa. Hii ni hafla ya kidini ndiyo
maana watu wa kidini wapo hapa. “Hakuna mahalipa kumaliza bifu kama hapa
kwenye shughuli ya kidini. Mfano, wangekuwa na Shehe Alhad
akawashikisha mikono si wangemaliza mambo yao?” alihoji mkazi mmoja wa
eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Hassan.
Balozi Seif Idd
KAULI YA BALOZI IDD
Alipopewa nafasi ya kuongea katika
shughuli hiyo, Balozi Seif Iddi alisema misikiti endapo itatumika kwa
mujibu wa maelekezo ya Mtume Muhammad itaendelea kuwa kimbilio la
waumini wote wa dini hiyo.
Makamu huyo wa rais, alisema kuwa, tabia
ya baadhi ya waumini wa dini hiyo kuifanya misikiti kuwa majukwaa ya
kisiasa ndiyo sababu kubwa inayoibua mafarakano katika jamii, yakiwemo
mambo ya kugombea uongozi misikitini. Balozi Idd aliongeza kuwa, waumini
na wananchi wanapaswa kujitahidi kuitumia misikiti mbali ya kusali
lakini pia inaweza kufanywa sehemu ya mipango ya maisha, sehemu ya kutoa
tiba, sadaka na michezo inayokubalika kiimani.
AGUSIA MADAWA YA KULEVYA
Pia kiongozi huyo wa ngazi ya juu
serikalini Zanzibar alisema jamii inaendelea kushuhudia matumizi yasiyo
sahihi ya matumizi ya madawa ya kulevya, udhalilishaji wa watoto wadogo,
wanawake na ujambazi. Pia akasema: “Kuporomoka kwa maadili hasa kwa
vijana kwa kiasi kikubwa kunatokana na kukosa fursa za kujifunza kupitia
misikiti ndani ya muongozo wa kiongozi wa dini ya Kiislamu, Mtume
Muhammad.”Shehe Zubeir
MUFTI MKUU NAYE ATOA NENO
Naye Mufti wa Tanzania, Shehe Zubeir
alisema inasikitisha kuona fursa kama hiyo ikiwa ni miongoni mwa nyingi
zilizopo kwa ajili ya kutekelezwa na waumini lakini wapo baadhi ya watu
wanaopiga vita. Alisema maendeleo yoyote, ikiwemo ya ibada yanapatikana
sehemu yenye ushirikiano na umoja.
Akasema mifarakano ni ugonjwa
unaostahili kuepukwa na Waislamu kwa vile inasababisha mtafaruku katika
jamii. ATOA TAHADHARI Mufti alitoa tahadhari akisema kwamba, waumini wa
dini ya Kiislamu iwapo hawatakubali kubadilika, Uislamu utaendelea
kubakia vijiweni tu.
KUHUSU ELIMU
Akigusia suala la elimu, Mufti alisema
kwamba, Uislamu na elimu ni kitu kimoja kinachomuwezesha mtu kupiga
hatua kubwa ya maendeleo.Dk. Bilal
MAKAMU WA RAIS MSTAAFU
Akitoa salamu zake katika Maulidi hiyo,
Dk. Bilal alisema mikusanyiko ya waumini ni darasa linalowasaidia
wahusika kuwa na upeo zaidi wa ufahamu wa dini yao. Dk. Bilal
aliupongeza uongozi wa Msikiti wa Majmuati Islamia chini ya Imamu Mkuu,
Shehe Alhad ambaye pia ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa uamuzi
wa kuandaa mkusanyiko huo aliosema unaongeza upendo, mapenzi na kujuana
miongoni mwa Waislamu.
WALIOALIKWA MAULIDI
Maulidi ya Uzawa wa Mtume Muhammad
(S.A.W) yaliyoandaliwa na uongozi wa msikiti huo, yalishirikisha pia
waumini wa madhehebu tofauti wa Tanzania, Kenya na wawakilishi wa
mabalozi na taasisi za kimataifa zilizopo nchini Tanzania.
WAGENI WAALIKWA WAONDOKA
Baada ya Shehe Alhad kuwasindikiza
wageni waalikwa, Wikienda lilimuweka chemba na kuanza kumuhoji kuhusiana
na kutofika kwa Diamond na Kiba ambao ilisemekana aliwaalika. “Aaah! Ni
kweli Diamond na Kiba niliwaalika na wote waliniahidi kufika lakini
nashangaa mpaka muda huu hawajatokea, sijui ni kwa nini lakini hilo
siwezi kulizungumzia zaidi isipokuwa hata mimi nashangaa,” alisema Alhad
na kuomba aachwe aendelee na majukumu yaliyombana, ikiwemo
kuagana na wageni wengine. Wikienda
liliwapigia simu Diamond na Kiba ili kutaka kujua kilichowasibu mpaka
kushindwa kutokea kwenye mwaliko huo.
DIAMOND: “Ni kweli nilialikwa, lakini nilipata dharura ya kifamilia, niko Afrika Kusini.”










Post a Comment