TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 08
Akiwa chini amekaa miguu ikiwa haina nguvu mkononi kulikuwa na ute mwingi wa yai ambalo halikuwa la kuku bali la mbuni kwa wingi wa ute.
Baada ya kupumzika kwa muda huku akiendeleza kupata mateso kutokana na kilio cha mtoto wa mbwa mwenye njaa kilichokuwa akilia yule msichana kwa utamu wa kuugegeda muhogo. Alinyanyuka pale chini na kurudi ndani japo ndani kilio cha mtoto wa kike kilishawishi kurudi kuangalie MJ anafanya machejo gani yenye kumfanya mtoto wa kike apagawe kiasi kile.
Japo sauti ile ilimshawishi arudi tena kupiga chabo, lakini yai alilojivunjia lilimfanya akimbilie bafuni ili kujiswafi kwani alikuwa ameloa sana kama gari lilikanyaga dimbwi la maji mengi yaliyomrukia na kumlowesha. Akiwa bafuni alipofungua maji ajimwagie alisikia maumivu makali pembeni ya jicho.
Alipokwenda kujiangalia kwenye kioo aligundua amechubuka baada ya kujikwangua ukutani bila kujua. Alijikuta akijitazama na kucheka mwenyewe kisha alirudi kuoga huku sehemu aliyojichubua ikiwa na mchubuko ilioonekana wazi.
Alirudi kukaa sebuleni kumsubiri MJ aliyekuwa akijilia vyake. Baada ya muda alitoka yule msichana akiwa ameongozana na MJ macho yakiwa yamemuwiva kwa utamu wa muhogo.
“Shemu siku nyingine.” alisema huku akielekea nje.
“Karibu tena,” Shuku alimkaribisha huku akimpiga jicho la wizi na kujisemea moyoni wenye fedha wanafaidi.
Baada ya MJ kumsindikiza mpaka nje alirudi ndani na kumuuliza rafiki yake:
“Vipi kitu umekionaje?”
“Mungu kakijalia kila idara kaka unafaidi tuache utani.”
“Mmh! Kawaida sema kuna mheshimiwa mmoja kaingilia penzi letu lakini huyu ndiye niliyetaka kumuoa.”
“Bonge la demu na kazi linaweza mtoto wa kike anajua kutumika na kuulilia,” Shuku alijisahau na kutaka kumwaga mtama kwenye kuku wengi.
“Shuku umejuaje? Unanipiga chabo nini?”
“Walaa, anaonekana tu mtu wa kudeka,” alipindisha ukweli.
“Na..na hapo jichoni vipi?” MJ alishtuka jeraha la Shuku.
“Nimejikwangua getini.”
“Si ungekwenda Dispensary uwekewe dawa kwenye jeraha?”
“La kawaida haliumi sana.”
“Sasa mi najipumzisha, mambo mengine utashughulikia mwenyewe.”
“Poa.”
Mj alirudi chumbani kwake na Shuku naye aliingia chumbani kwake kupumzika kuvuta muda.
****
Majira ya saa tatu na nusu usiku waliingia Bills, baada ya kuingia ndani ya ukumbi macho ya Shuku yalitazama kila kona huenda kamuona yule msichana aliyemchanganya jana yake lakini macho yake yalitoka kapa na kujikuta akianza kuichukia siku ile.
Walikwenda kutafuta sehemu ya kukaa na kuagiza vinjwaji, wakati wote macho ya Shuku alitembea kama setilite kumsaka mrembo wa jana yake. Siku zote MJ hakuwa anatulia sehemu moja kila alipoingia kwenye kumbi za starehe.
“Shuku mi nazunguka kidogo maana kukaa sehemu moja siwezi.”
“Poa, wee nenda mi nipo.”
“Shuku acha ushamba zungukazunguka kidogo ili kusafisha macho unaweza kupata demu wa kula naye raha.”
“Hata nikimpata si mpaka nikufuate unipe mkwanja?”
“Ooh! Nilisahau,” MJ alitoa pochi na kumkatia laki mbili.
“Hizi zinakutosha kama hazitoshi utaishtua.”
“Poa.”
MJ aliachana na Shuku na kuteremka chini na kumuacha akipiga ulabu macho yake yakiwa na shauku ya kumuona yule mwanamke. Pamoja ndani ya Bilicanas kulikuwa na wanawake wengi wazuri wenye maumbile ya vishawishi vya ngono kwa wanaume marijali, lakini Shuku macho yake hayakuwaona zaidi ya kumtafuta yuleyule mwanamke kama kipofu aliyeahidiwa kuona.
Baada ya kunywa kidogo aliamua na yeye kuteremka chini ambako kulikuwa na msanii wa kizazi kipya Dully akiporomosha burudani ya kufa mtu. Kila mmoja alikuwa akirukaruka kutokana na Dully kuwapeleka puta. Shuku akiwa na bia mkononi wakati akijichanganya kwenye kundi la watu waliokuwa wakiondoka sambamba na Dully.
Aliamua na yeye kufurahia siku ile kwa kuamini siku ya pili atakwenda maeneo anayokaa yule demu na gari kali amng’oe kwa upole. Wakati akicheza kwa bahati mbaya alimkanyaga dada mmoja na kujikuta akigeuka kumuomba radhi wakati huo muziki ulikuwa umenyamaza.
Macho yake yalipatwa na mshtuko baada ya kukutana na mtu aliyekuwa na hamu ya kumuona.
“So..so..rry mrembo,” alipatwa na kigugumizi.
“Mmh, He! ni wewe tena?” yule msichana alimuuliza kwa kumshangaa.
“Haikuwa dhamira yangu,” Shuku alijitetea.
“Mmh! Mbona unajitetea sana kama nimekulaumu?” Yule mwanamke alizidi kumshangaa Shuku.
“Najua nimekuumiza.”
“Kaka wee aliyeniumiza hakujitetea kwa vile alikuwa ndo ananiingiza dunia ya wakubwa, sasa hivi wanakula wengine wala hana habari.”
“Basi...na..na.”
“Wee kaka vipiii? Usinigeuze mwalimu wa chekechea ninayefundisha watu kusoma, hebu nyoosha maneno nitakuelewa tu.”
“Ni..ni..nili...” Shuku alijikuta akimung’unya maneno.
“Mmh! Makubwa, sasa fanya hivyo nipe simu yako,” yule msichana alisema huku akinyoosha mkono.
Shuku kwa haraka alitoa simu ambayo ilikuwa ya bei mbaya aliyonunuliwa na MJ alingane na yeye.
“Mmh! Unatisha unatembea na kiwanja mkononi,” msichana alichanganyikiwa kuiona simu ya milioni moja na nusu aliyokuwa nayo Shuku.
“Mbona mambo ya kawaida tu,” Shuku alicheka kicheko cha dharau cha kujiamini.
“Sasa hii ndiyo namba yangu naomba kesho tuwasiliane,” yule msichana alisema huku akimrudishia simu Shuku.
“Leo vipi?”
“Nipo na mtu na jamaa mtata ile mbaya.”
“Poa basi mrembo, ya vocha,” kwa kuchanganyikiwa Shuku alimpa laki mbili zote alizopewa na MJ.
“Asante baby,” yule msichana naye alichanganyikiwa na kujikuta akimbusu na kuachana naye kurudi kwa mjanja wake aliyekuwa mezani akinywa.
Shuku alikuwa kama yupo ndotoni, kabla ya kuondoka yule msichana alifikicha macho ili kupata uhakika kweli kakutana na yule mrembo. Bado hakukubaliana na kilichotokea alijifinya kidogo na kusikia maumivu na kuamini kweli kilichotokea mbele yake ni cha kweli wala si ndoto.
Akiwa bado amesimama yule mwanamke alipita mbele yake akiwa ameongozana na mwanaume ambaye hakuwa mgeni alikuwa jamaa wa siku zote. Wakati wakitoka yule msichana aliugeuka nyuma na kusema kwa ishara.
“Kesho basi.”
“Poa.”
Walitoka nje na kumwacha Shuku akiwa bado amesimama palepale kama sanamu akimsindikiza kwa macho na kuuapia moyo wake siku atakayomtia kwenye himaya yake atamaliza ufundi wote kuhakikisha akionja achonge mzinga kabisa.
Akiwa bado yupo katikati ya dimbwi la mawazo simu yake iliita, alipoangalia alikuwa ni MJ. Alipokea:
“Haloo vipi?”
”Upo wapi?”
“Chini.”
“Basi nilijua bado upo juu.”
“We upo wapi?”
“Nipo juu.”
“Poa nakuja.”
“Noo, nakuja hukohuko nataka tuondoke kuna demu wangu mmoja wa chuo kanipigia simu yupo home ananisubiri.”
“Hakuna tatizo nakusubiri.”
Shuku alikata simu na kukumbuka alikuwa hajasevu ile namba ya mrembo.
“Ooh! Shit,” alipiga kelele peke yake baada ya kugundua namba imefutika.
Alitoka nje mbio labda atamuwahi lakini alipofika nje aliiona gari ndo inaondoka. Alijikuta akichuchumaa na akipiga ngumi chini na kujiona bwege namba moja. Simu yake iliita tena alipoangalia ilikuwa ya Mj na kujikuta akiongezwa hasira.
Hakuipokea aliendelea kuchuchumaa akitamani kulia kwa kuamini amepoteza alichokitafuta kwa muda mrefu.
MJ baada ya kumtafuta kwa muda mrefu sehemu aliyomuelekeza kisha kumpigia simu iliyoita bila kupokelewa, aliamua kutoka nje ili aondoke kwa kuamini Shuku alikuwa na fedha ya kutosha ya kuweza kukodi teksi kwa muda ule mpaka nyumbani.
Alipotoka nje alishangaa kumuona rafiki yake akiwa amechuchumaa chini mkono mmoja kashika chini na mwingine kashikilia simu.
Alimshangaa rafiki yake na kujiuliza mbona yupo vile, wasiwasi wake labda pombe zimemzidia na pale alipochuchumaa alikuwa akitapika. Alimsogelea na kumshangaa kumkuta rafiki yake akipiga ngumi chini huku akijilaumu.
“Shuku vipi?”
“Wee acha, mimi bonge la fala.”
“Bonge la fala! Una maana gani?”
“Yaani nimefanya bonge la mistake.”
“Mistake gani tena, umeibiwa?”
“Hapana.”
“Umefanya kosa gani lililokuchanganya?”
“Si yule demu.”
“Eeh! Kafanya nini?”
” ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA
TOROJO BAMIA (Winga teleza) - SEHEU YA 1 - 8
#Hakika si ya kukosa hii SIMULIZI.
SEHEMU YA 1>>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEMU YA 2: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEMU YA 3:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEMU YA 4:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEMU YA 5==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
SEHEMU YA 6: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-06.html
SEHEMU YA 7==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-07.htm
SEHEMU YA 8==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-08.html
Utamu ndio kwanza unazidi kukolea. Bado sehemu kibao kuweza kuisha chombezo hili la aina yake .
Kamwe usithubutu kusimuliwa hii ENDELEA KULIKE HAPA ========================>www.facebook.com/2jiachie: Utamu ndio kwanza unazidi kukolea. Bado sehemu kibao kuweza kuisha chombezo hili la aina yake . Kamwe usithubutu kusimuliwa hii simulizi ingia ujisomee mwenyewe hapa hapa uwanja wa simulizi pekee.
:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.
Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.

Post a Comment