FUTA MACHOZI MPENZI-06
NYEMO CHILONGANI
KWA WASOMAJI WAPYA
Mtoto wa bilionea mkubwa, mwenye sura nzuri, Melania anajikuta akiwa mikononi mwa mvulana ambaye ni mtoto wa waziri mkuu, Nicolaus. Wanaanza kupendana, wanaangaliana sana, kila mmoja anamuona mwenzake kuwa wa thamani sana.
Nicolaus alivumilia, hakutaka kumwambia Melania kwa sababu alimuogopa. Moyo wake uliteseka sana lakini mwisho wa siku akaamua kumwambia msichana huyo ukweli kwamba alikuwa akimpenda sana kutoka moyoni mwake na hivyo kuambiwa asubiri kwani lilikuwa jambo la kujifikiria.
Wakati hayo yakiendelea, upande wa pili kuna mvulana mwingine anayeitwa William. Huyu alizaliwa na mwanamke masikini aitwaye Sophia. Maisha yao yanakuwa na umasikini mno lakini mbali na hayo yote, huyu William alikuwa na sura mbaya.
Watoto wengi walikuwa wakimuogopa, kila alipokuwa akitabasamu, ubaya wa sura yake ulikuwa ukiongezeka maradufu. Pamoja na sura yake mbaya, ila William alikuwa na akili mno. Darasani, alikuwa mtu wa kwanza, alifaulu vema masomo yake kiasi cha mama yake kumshukuru Mungu kila siku.
Unajua nini kiliendelea?
SONGA NAYO...
Hakujua ni kitu gani alitakiwa kumwambia Nicolaus, ni kweli alikuwa akimpenda lakini hata naye alikuwa akimuogopa. Usiku mzima ulikuwa ni kujifikiria ni jibu gani alilotakiwa kumpa kijana huyo aliyekuwa akilisubiria kwa hamu kubwa.
Asubuhi ilipofika, akaelekea shule. Alipofika huko, hakutaka kuonana naye, hakutaka kumpa upenyo wa kuzungumza naye kwani alimpenda lakini hakuwa tayari kumwambia kwa mdomo wake.
Nicolaus hakulalamika, moyo wake haukuwa ukijiamini kabisa, ni kweli alikuwa akilisubiri jibu hilo kwa nguvu zote lakini naye aliogopa kumfuata msichana huyo na kumuuliza kuhusu jibu lake.
Siku zikakatika, ukaribu wao ukapungua kwa kuogopana kwani muda huo mioyo yao ilikuwa na kitu cha tofauti kabisa, hakukuwa na urafiki tena bali kilichokuwa kikiibuka kilikuwa ni mapenzi ya dhati.
Mwaka huo ukapita na kuingia kidato cha nne. Mwaka huo wa mwisho ndiyo ambao Nicolaus akalikumbushia lile jibu alilotakiwa kupewa na moja kwa moja msichana huyo kukubaliana naye na hivyo kuanza uhusiano wa kimapenzi uliotakiwa kuwa siri kubwa.
Wakawa wapenzi, wakapenda sana, kila siku walikuwa pamoja, walionyesheana ni kwa jinsi gani walikuwa wakipendana. Wakati uhusiano huo ukiendelea, mama yake Melania, Pamela akapata mtoto wa pili wa kiume na kumpa jina la James ambaye aliiongeza furaha iliyokuwa katika familia hiyo.
Maisha yaliendelea kama kawaida. Wanaume hawakuwa mbali na Melania, walimpenda kwani alikuwa msichana mrembo ambaye kila mmoja hakuamini kama katika maisha yake angekutana na msichana mrembo kama alivyokuwa Melania.
Japokuwa walikuwa kwenye uhusiano wa dhati, Melania hakutaka kufanya mapenzi na Nicolaus. Kila siku mwanaume huyo alipomwambia wakafanye, msichana huyo alikuwa akitoa sababu nyingi kwamba yupo bize na wangefanya siku nyingine.
Hilo likamuumiza sana Nicolaus, kila alipomwangalia mpenzi wake, jinsi alivyonawiri mwili wake ulimsisimka, mapigo yake ya moyo yalimdunda kwa nguvu kwani alitamanisha na kuvutia kuliko kawaida.
“Kama hataki si bora nimbake tu,” alisema Nicolaus huku akionekana kushikwa na mhemko mkubwa kwa msichana huyo.
Hilo ndilo alilolipanga, hakutaka kuona akiendelea kula kwa macho na wakati msichana huyo alikuwa mpenzi wake. Walikuwa wakifanya mambo mengi, wakishikana hapa na pale, wakibadilishana mate lakini kufanya mapenzi lilionekana kuwa suala gumu sana.
“Kwa hiyo hutaki?” aliuliza Nicolaus.
“Si kwamba sitaki baby!”
“Kumbe?”
“Nataka ila muda bado!”
“Kwa hiyo mimi niendelee kuwa mpenzi mtazamaji tu?” aliuliza Nicolaus.
“Simaanishi hivyo!”
“Kumbe unamaanisha nini? Sasa kama hatufanyi mapenzi, kitu gani kitatutambulisha kwamba mimi na wewe ni wapenzi? Kuna utofauti gani wa mimi na kaka yako au wewe na dada yangu?” aliuliza Nicolaus huku akionekana kupagawa.
“Utofauti upo, tunabadilishana mate, hiyo ni ishara mojawapo ya kwamba sisi ni wapenzi,” alijibu Melania.
“Hiyo haijatosha. Au unatembea na jamaa fulani halafu kwangu unanikazia?” aliuliza Nicolaus.
“Hapana! Wasiwasi wako tu!”
Kabla hajapanga kumbaka msichana huyo, mara kwa mara Melania alikuwa akifika nyumbani kwao na kuingia mpaka chumbani kwake lakini baada ya kuwa na wazo la kumbaka, tayari kukawa na ugumu kwa msichana huyo kufika nyumbani kwao.
Mara kwa mara alikuwa akimwambia Melania afike nyumbani kwao lakini msichana huyo aligoma, ni kama alikuwa ameshtukia kile kilichotaka kutokea huko. Nicolaus hakutaka kubaki kimya, kila siku ilikuwa ni lazima amkumbushe kwamba alitaka kuzungumza naye nyumbani kwao.
Uhusiano huo uliendelea mpaka walipomaliza kidato cha nne na kusubiri matokeo ya kuingia kidato cha tano. Hawakuwa na hofu, walijua kwamba wangefaulu kwani shule waliyokuwa wakisoma ilikuwa miongoni mwa shule bora zilizokuwa zikifaulisha sana ingawa ilikuwa ni ya watoto wa matajiri tu.
Walisubiri nyumbani huku kila mmoja akifikiria lake. Nicolaus, alikuwa akifikiria kufanya mapenzi na Melania na wakati msichana huyo alikuwa akifikiria kuhusu elimu yake ya kidato cha tano na sita.
Waliendelea kuwasiliana. Kila siku kwa Nicolaus iilikuwa ni malalamiko tu, alimtaka mpenzi wake wafanye mapenzi lakini msichana huyo alikataa katakata na kumwambia kwamba alitakiwa kusubiri hadi ndoa. Ilimuuma, hakuwa na jinsi, kwa sababu aliambiwa asubiri, akafanya hivyo.
Wakafaulu vizuri na kuingia kidato cha tano. Wakati wakijiandaa kusoma kidato cha tano Tanzania, baba yake Nicolaus akaamua kumsafirisha mtoto wake aelekee nchini Australia katika Jiji la Melbourne kuendelea na masomo ya chuo katika Chuo cha Monarch kilichokuwa jijini humo.
“Mpenzi! Nitakuwa muaminifu katika kipindi chote nitakachokuwa huko,” alisema Nicolaus.
“Na mimi pia nitakuwa mwaminifu katika kipindi chote nitakachokuwa huku,” alisema Melania.
Wakaagana na Nicolaus kupanda ndege na kuelekea nchini Australia. Huku nyuma Melania alikuwa na mawazo tele, kila siku alikuwa akiwasiliana na Nicolaus na kumwambia namna alivyokuwa akimpenda.
Alikosa furaha, kila alipokuwa akilala usiku picha ya mwanaume huyo ilikuwa ikimjia kichwani mwake. Miaka ikakatika, miaka miwili ikapita na kuanza masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alifurahi kuingia chuoni humo. Siku za kwanza alikuwa gumzo, kila mwanaume aliyekuwa akimwangalia alitokea kumpenda. Alikuwa mtoto wa bilionea mkubwa, mwenye kampuni nyingi na hata maisha yake hapo chuoni yalionyesha kwamba alikuwa mtoto wa bilionea.
Alikuwa akiendesha gari la thamani kuliko hata maprofesa wenyewe. Kila alipokuwa akiingia chuoni, wote walikuwa wakilishangaa gari lake ambalo dukani lilikuwa ni zaidi ya milioni mia moja na hamsini.
Hakujali, kwake, fedha ilikuwa kawaida sana. Hakuwa mtu wa matanuzi, alipendwa na watu wengi kwa kuwa alikuwa mcheshi na kutokana na uzuri wake ilikuwa vigumu kugundua kwamba mpaka kipindi hicho hakukuwa na mwanaume aliyemuingia kimwili.
Wakati akiwasiliana na Nicolaus kwa kipindi chote ndipo akamwambia kwamba alitarajiwa kurudi nchini Tanzania kwa ajili ya likizo fupi. Melania akafurahi sana, hakuamini kama kweli kipindi hicho angemuona mpenzi wake kwa mara nyingine.
Akajipanga kumpokea kwa mapenzi mazito. Baada ya kuwasiliana kwa siku kadhaa hatimaye mwanaume huyo akaingia Tanzania. Walipoonana, hakuonekana kuwa kawaida, yale mapenzi ambayo aliyaona kwa mpenzi wake kipindi cha nyuma hayakuwa kama kipindi hicho.
Melania alishangaa, alimfahamu Nicolaus, alipokuwa na furaha, alimjua vilivyo na hata alipokuwa amebadilika, aliweza kuligundua hilo. Hakujua tatizo lilikuwa nini. Hilo lilimchanganya kichwani mwake, wakati mwingine alihisi kwamba kwa sababu alishindwa kufanya naye mapenzi basi ndiyo maana aliamua kubadilika namna hiyo.
Hakuwa akizungumza naye hata kwenye simu, muda mwingi mwanaume huyo alimwambia kwamba alichoka. Alipokuwa akichati naye katika Mtandao wa Allo, ulionyesha kwamba meseji zilikuwa zikisomwa lakini hazikuwa zikijibiwa.
“Nicolaus, tatizo nini mpenzi?” aliuliza msichana huyo.
“Hakuna tatizo!”
“Niambie ukweli! Sipendi kukuona ukiwa kwenye hali hii! Wewe niambie tatizo nini?” alisema Melania, wakati huo walikuwa wakizungumza kwenye simu.
“Hutaki hata tufanye mapenzi! Sawa, umenifanya kula kwa macho, lakini hata kunionyeshea umbo lako mpenzi,” alisema Nicolaus.
“Kwa hiyo hilo ndilo linalokufanya kuhuzunika namna hiyo jamani?”
“Ndiyo! Umeumbika lakini hunipi hata nafasi ya kukuona, kweli mpenzi unanifanyia hivi!” alilalamika Nicolaus.
“Basi subiri!”
Baada ya dakika kadhaa, picha kadhaa zikaingia katika simu ya Nicolaus, akazifungua na kuanza kuziangalia. Zilikuwa picha za utupu za msichana huyo, alijipiga pasipo kuwa na aibu yoyote ile.
Hakuogopa, alimwamini sana Nicolaus, kumtumia picha za utupu tena zilizoonyesha sura yake hakuona kuwa na tatizo lolote lile. Nicolaus alipozipata picha hizo, akakenua, moyo wake ukawa na furaha sana.
“Sasa amekwisha...” alisema Nicolaus.
Kuanzia kipindi hicho, hakutaka kuwasiliana tena na Melania. Ndiyo kwanza akaondoka kurudi nchini Australia huku moyo wake ukiwa na furaha tele. Kiukweli alikuwa na kazi kubwa na picha hizo, kitendo cha kutumiwa tu, lilikuwa kosa kubwa kwa msichana huyo.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumamosi mahali hapa.

Post a Comment