KAULI YA KWANZA YA KOCHA MPYA WA AZAM FC AMBAYE AMECHUKUA NAFASI YA ZEBEN
Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, mchana huu imemtangaza, Aristica Cioaba, kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.
Cioaba,
45, raia wa Romania anakuja Azam FC kurithi mikoba ya Mhispania Zeben
Hernandez, aliyesitishiwa mkataba pamoja na benchi lake zima la ufundi.
Kwa
upande wake Cioaba, alisema kuwa anafuraha kubwa leo hii kusaini
mkataba wa kuifundisha timu hiyo huku akiahidi kazi nzuri na kuifanya
timu hiyo kuwa bora.
“Najua
Azam FC hapa Tanzania ni moja ya timu kubwa yenye historia huko nyuma,
napenda kuushukuru uongozi kwa kuniamini na kunipa nafasi kuja
kufundisha soka kwenye nchi hii, kwa mashabiki napenda kuwaambia kuwa
nalijua soka la Afrika, nimewahi kufundisha Ghana na kupata matokeo
mazuri.
“Kuhusu
wakati ujao, nina furaha sana kuhusu uongozi walipoongea na mimi wakati
tunaweka mipango ya timu ya hapo baadaye na hili ni jambo zuri kwa
kocha, kitaaluma nawaahidi mashabiki na watu wote wanaoipenda Azam FC,
niko hapa kuwapa mambo mazuri katika kazi yangu kwenye klabu,” alisema.
Msimu
uliopita, Cioaba aliiongoza Aduana Stars ya Ghana kushika nafasi ya
pili kwenye Ligi Kuu ya Ghana, ambapo anafahamiana kwa ukaribu na nyota
wawili wa Azam FC, Yakubu Mohammed na Yahaya Mohammed, waliosajiliwa
kutoka timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo.
Mbali
na kufundisha soka nchini Ghana pia amewahi kufanya kazi kwenye miamba
ya Morocco, Raja Casablanca, Al Masry ya Misri na katika nchi za
Romania, Kuwait, Oman na Jordan.
Post a Comment