EXCLUSIVE: OKWI AVUNJA MKATABA WAKE DENMARK, SONDERJYSKE YASEMA ISHU IMEANZIA KWENYE NAMBA
Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ameamua kuondoka nchini Denmark.
Okwi amevunja mkataba wake na klabu ya Sonderjyske Fodbold ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.
Mkuu
wa masuala ya michezo ya klabu hiyo, Jorgen Haysen amesema Okwi mwenye
umri wa miaka 24 ameamua kuvunja mkataba baada ya kuona hajapata namba
ya uhakika katika kikosi hicho.
“Okwi
hakupata nafasi ya kucheza kama ambavyo alitarajiwa, lakini kiwango
chake pia hakikukua kumshawishi kocha aanze kumpa nafasi kwa kiwango cha
juu.
“Mwisho akaamua kuondoka, tumekaa na kufikia makubaliano vizuri. Zaidi, ninamtakia kila la kheri aendako,” alisema.
Okwi alitua katika kikosi hicho Julai 2015 akitokea Simba na kusaini mkataba wa miaka mitano na mkataba wake ungeisha 2020.
Hata hivyo, mara kwa mara Okwi amekuwa akihusishwa kurejea Simba lakini amekuwa haeleweki.
Mara kadhaa, amekuwa akikanusha na mara nyingine akieleza yuko tayari kuzungumza au yuko tayari kurejea Simba.
Hata
hivyo, viongozi wa Simba wamekuwa kwenye mgawanyiko mkubwa kuhusiana na
ujio wake, wako wakitaka arejee na wengine wakipinga kabisa.
Post a Comment