Boyence Apigwa Mimba ya 2, Kwa sasa Ana Mimba Ya Miezi Minne
Beyonce Knowles.
IMETHIBITIKA kuwa mwanamuziki wa
R&B, Beyonce Knowles ana mimba ya miezi minne baada ya kipande cha
video kusambaa kikionesha mimba hiyo. Kwa mujibu wa mtandao mkubwa wa
Showbiz, umeanika kipande hicho cha Beyonce na kueleza kuwa, staa huyo
anayetamba na Albamu ya Lemonade anatarajia kupata mtoto wa pili kwa
mumewe, Shawn Carter ‘Jay Z’ na hakutaka kuweka hadharani hadi
atakapokaribia kujifungua.
Beyonce Knowles.
Katika kipande hicho alichoachia
mtandaoni na kufuta haraka, kinamuonesha Beyonce akiwa katika kampeni ya
mavazi yake aliyoyaita jina la mtoto wake, Blue Ivy yanayotambulika
kama Ivy Park. Mashabiki wake wengi wa kwenye mitandao ya kijamii
ikiongozwa na Twitter wamempongeza Beyonce na ujauzito huo. Kwa muda
mrefu kumekuwa na tetesi za ujauzito wake japo hakukuwa na picha
zilizoonesha na sasa imeonekana wazi. apigwa mimba ya 2
Post a Comment