ad

ad

Lulu Diva Atambulisha Wimbo Wake wa ‘Milele’ Global TV



 MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva, amegeukia upande wa pili wa Bongo Fleva kwa kuibuka na ngoma yake ya kwanza aliyomshirikisha Barnabas Elias maarufu ‘Barnaba. 
 
Wimbo wake huo umetungwa na msanii wa Bongo Fleva, Barnaba na kutengeneza katika studio ya Barnaba. Katika mahojiano na Global TV Lulu Diva amesema mashabiki wake waliomzoea kumuona katika video mbalimbali kwa sasa watarajie ngoma kali kutoka kwake kwa sasa ameanza na Milele na hivi karibuni ataachia video ya wimbo wake aliyoitengenezea Afrika Kusini.  Ametumia zaidi ya milioni 40 kutengeneza ngoma hiyo.

Pia amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva ndani na nje ya nchi kudownload wimbo wake kupitia Mkito au Youtube.


No comments

Powered by Blogger.