ad

ad

HAYA MANENO HAYA YA KOCHA WA AZAM KUHUSIANA NA YANGA, TUSUBIRI...


Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, raia wa Hispania, amesema endapo kikosi chake hakitakumbwa na majeruhi wengi katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, basi wana asilimia kubwa ya kuivua Yanga ubingwa wa ligi hiyo.

Azam ambayo katika mzunguko wa kwanza imemaliza ikiwa nafasi ya tatu na pointi 25 ikipitwa pointi kumi na vinara Simba, imejinasibu kutokana na usajili ilioufanya.

Timu hiyo katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo, imewaongeza Waghana watatu ambao ni Samuel Afful, Yahaya Mohammed na Enock Agyei, huku pia ikimsajili mzawa, Joseph Mahundi.

Zeben amesema: “Kuna mabadiliko makubwa nimeyaona katika kikosi changu, lakini kikubwa ambacho nahofia ni uwepo wa majeruhi, kama sitakuwa na majeruhi wengi, basi mzunguko wa pili natarajia kufanya vizuri zaidi na kuchukua taji la ligi.

“Kuachwa mbali na waliopo juu yangu si tatizo kwani natambua kwamba mzunguko wa pili tutacheza mechi nyingi nyumbani, hivyo tutahakikisha tunakusanya pointi tatu katika kila mchezo wetu.”

No comments

Powered by Blogger.