HASIRA ZA YANGA ZINAWEZA KUFANANISHWA NA FARU JOHN KWA SIMBA
JUMATATU na Jumanne ya wiki hii, wachezaji wa Yanga waligomea kufanya mazoezi kwa kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wakidai mishahara yao, mashabiki wa timu hiyo wakapata presha kubwa kwa kuwa tukio hilo limetokea wakati ndiyo kwanza raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara imeanza.
Ikabidi yafanyike ‘mafekeche’ kwa viongozi wa Yanga kupambana juu chini kuhakikisha wachezaji wao wanatimiziwa mahitaji yao wanayodai ili kurejea kwenye majukumu yao kama kawaida.

Taarifa za uhakika ambazo Championi Ijumaa limezipata ni kuwa kila kitu kimerejea kwenye mstari na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amethibitisha kuwa sasa hivi mambo ni safi na morali yao imerejea kwa kiwango cha juu na kuwataka Wanayanga kujitokeza kwa wingi uwanjani leo Ijumaa katika mchezo dhidi ya Afrikan Lyon kwa kuwa hasira zao hazipimiki.
Gazeti hili lilifika katika mazoezi ya Yanga, jana na juzi na kushuhudia jinsi wachezaji hao walivyo na morali ya juu huku baadhi yao wakitamba kuwa kuonyesha wana hasira wanaanza na Lyon kisha wengine wanafuata.
Hasira za Yanga zinaweza kufananishwa na Faru John, mnyama ambaye katika siku za hivi karibuni amesababisha gumzo nchini huku ikielezwa kuwa baadhi ya tabia zake ni kuwa na hasira kali, kutotaka kuona mwingine akitawala, kutaka kuwa mfalme popote
pale anapokuwa kama ambavyo Yanga inataka kuendelea kutawala soka la Tanzania.
Lyon itapata kazi ngumu Yanga inashika nafasi ya pili katika ligi kuu ikiwa na pointi 36, itakutana na Lyon inayoshika nafasi ya 12, ikiwa na pointi 18.
Katika mazoezi ya jana asubuhi ya Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru, Kocha wa Yanga George Lwandamina kwanza alikuwa mkali kwa wachezaji wake, pili alitumia muda mwingi kuwaelekeza mbinu za mfumo kisha akagawa vikosi viwili, kimoja kikiwa ni kile ambacho anatarajiwa kukianzisha kwenye mchezo wa leo. Kikosi cha leo & pasi za nyuma Kutokana na mazoezi hayo Lwandamina anatarajiwa kuanza na kikosi hiki leo:
Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Said Makapu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Deus Kaseke. Wakati mazoezi yakiendelea, kocha msaidizi wa timu hiyo, Mzambia,
Noel Mwandila, alikuwa akiwazuia wachezaji kupiga pasi za nyuma wakati timu inapokuwa na mpira na alikuwa akipiga filimbi ya faulo kwa timu itakayopiga pasi ya nyuma. Kocha afunguka Baada ya mazoezi hayo, kocha mwingine msaidizi, Juma Mwambusi alisema morali ya wachezaji ipo juu na kusisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.
Ngoma, wenzake kukosa mchezo Mwambusi alisema wachezaji Ally Mustapha ‘Barthez’, Matheo Anthony na Donald Ngoma watakosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi lakini habari za uhakika ni kuwa Ngoma yupo fiti ila ana kadi tatu za njano na ndiyo maana hatakiwi kucheza mchezo huo.
Tujikumbushe Faru John Akiwa katika ziara ya kikazi Ngorongoro, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliibua sakata la kuhamishwa kinyemela faru huyo aliyeletwa nchini akitokea Afrika Kusini na kudaiwa kupelekwa Grumet. Waziri mkuu alitaka ukweli kuhusu upotevu wa Faru John ambapo inadaiwa aliuzwa kinyemela kwa shilingi milioni 200 huku wauzaji wakipewa shilingi milioni 100 kama kianzio.

Post a Comment