VIONGOZI SIMBA WAONA HII SASA NI KERO, WAAMUA KUACHANA NA MKUDE
Katika
siku za hivi karibuni kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye
mkataba wake na timu hiyo unafikia tamati mwezi Januari mwakani, alisema
kuwa mpaka sasa haelewi chochote kama ataendelea kuitumikia timu hiyo
au la.
Kutokana
na hali hiyo, Mkude akawataka Yanga wakamsajili kama kweli wanamhitaji
akidai bila kusita atasaini timu hiyo, kwani yupo tayari kuitumikia.
Jambo
hilo linadaiwa kuukera uongozi wa Simba na umeamua kuchukua jukumu la
kukaa kimya bila ya kumfuatilia tena kiungo huyo na wamesema kama
anataka kwenda Yanga aende.
“Mkude
hivi sasa anatakiwa kuwa makini sana, vinginevyo anaweza kujikuta
katika wakati mgumu kwani uongozi umesema kuwa hautahangaika naye tena,
yeye kama anataka kuondoka basi aondoke zake.
“Wamefikia
hatua hiyo baada ya kumbembeleza sana kusaini mkataba mpya lakini yeye
amekuwa akizingua akidai kuwa fedha anazotaka kupewa ni kidogo lakini
pia kila akiitwa kwa ajili ya mazungumzo amekuwa akikataa,”
kilisema chanzo chetu cha habari na kuongeza:
“Kutokana
na hali hiyo uongozi wa timu unamsubiria kocha aje ili uweze kuzungumza
naye na ikiwezekana aanze kuwa anamtumia Mzamiru Yassin kama kiungo
mkabaji halafu Juma Awadh awe anacheza namba nane.”
Alipotafutwa
Mkude ili aweze kuzungumzia hali hiyo alisema: “Kama wamefikia uamuzi
huo ni wao lakini binafsi kwa sasa siwezi kusema chochote juu ya suala
hilo.”
Post a Comment