Rais Magufuli alivyompigia simu Makonda katikati ya mkutano wa Hadhara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli jana alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika ziara yake kwa kusikiliza kero za wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Rais
Dkt Magufuli alitoa pongezi hizo alipompigia simu Mkuu wa Mkoa wakati
akiwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi katika maeneno ya
Ubungo jijini Dar es Salaam.
“Endelea
hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine
ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu
ya kuja kuuliza maswali kui kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za
Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri
mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali
makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” alisema Rais Magufuli.
Post a Comment