Dume Suruali Darasa Kwa Kizazi Cha Digitali
Dume Suruali
Na John Joseph
WIMBO wa Dume Suruali ndiyo
inawezekana ukawa msemo kwa Watanzania wengi kwa kipindi cha miezi kadhaa ijayo,
hiyo ni kutokana na mashairi yaliyoandikwa na mtunzi wa wimbo huo, Mwana FA akimshirikisha
V-Money.
Unazungumzia mwanaume
anavyolalamika kulazimishwa kuhonga fedha kwa mwanamke. Mwan FA ambaye jina
lake halisi ni bwana Hamisi Mwinjuma, amezungumza na gazeti hili kufafanua kile
alichokiandika kwenye wimbo huo aliomshirikisha bi Vanessa Mdee:
Lengo lako hasa ni nini?
Ni kuwataka watu wasiwe
wajinga kwa kuwa mapenzi ni hisia na siyo biashara. Matukio kama hayo yamekuwa
yakitokea mara nyingi tu katika kizazi cha sasa. Sina maana ya kuwasema vibaya
wanawake lakini tukumbuke hata upande wetu sisi wanaume kuna Malioo ambao wao
wanapenda kuhongwa na wanawake, ujumbe huu ni maalum kwa pande zote.
Kwa nini Vanessa?
Vanessa ni aina ya wanawake
ambao sisi wanaume tukimuona tunahisi ili umpate ni lazima umuhonge sana,
sababu ya kumchagua yeye ni kwa kuwa anawakilisha vizuri wasichana wa aina hiyo
ambao wengi wamekuwa na mitazamo hiyo.
Umetunga kwa kuwa yamekutokea?
Mimi ni msanii, nawakilisha
mengi yanayotokea kwenye jamii, yapo yaliyonitokea na mengine watu wangu wa
karibu na jamii kwa jumla, kuna vitu ambavyo unaongeza ili sanaa ikamilike
lakini kwa ufupi nimezungumza ukweli.
Utunzi wa wimbo ulikuwaje?
Niliutunga ndani ya muda wa
siku moja niliyoenda studio lakini ilinichukua mwezi mzima kuwa naurekebisha
hapa na pale. Hata Vanessa nilipomweleza alikubaliana na wazo langu na kuamini
utafanya vizuri.
Kwa nini ulichagua MJ Records?
Prodyuza wa wimbo huo ni Daxo
Chali ambaye ni mdogo wake Marco Chali. Nilienda MJ kwa Marco nikamueleza
nataka kazi fulani akanipa ‘beat’ mbili, nikachagua yangu na Vanessa naye
akachagua hii ambayo ndiyo imetumika kwenye wimbo.
Tuliamua kuchagua hiyo kwa
kuwa Vanessa alinishauri ni beat laini ambayo kwanza itakuwa na ladha tofauti
ndiyo maana tukaitumia.
Umemtaja tajiri Salah kwenye wimbo, ni nani?
Huyu ni rafiki yangu wa
karibu, ni mmoja wa watu wangu ambaye amekuwa anashangaa sana jinsi wanaume
wanavyohonga.
Mashairi ya Dume Suruali
Mwana FA
Hudat hudat hii ni salam na
ufahamu
Kama unauza mapenzi siyo kwa
binamu
Huna haja ya kusubiri hii ni
hukumu
Hakuna kitu utapata utangoja
kama askari wa zamu
Dume suruali dume kaptula
Shauri zako ilimradi sipati
hasara
Usione utani me sihongi hata kwa
ishara
Utaniambia nini mpaka
unigeuze fala
Kwanza nasikia hongo zinaleta
mkosi
Sentano yangu hugusi hata ukiongea
kidosi
Yabaki mapenzi tusileteane
ujambazi
Hata upige sarakasi utachonga
viazi.
BAHILI KAMA NINI!!!!!!!!! Ndiyo
mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii
tena
Kwani unauza nini dada!
Hunitakii mema.
Kiitikio
We dume suruali kaa mbali
nami
Kama dume suruali kaa mbali
nami
Huendani na mimi
I want Gucci, Fendi, spend it
on the girl like me
My name is Vee Money, money
spend on the girl like me
MWANA FA
Nihonge nanunua nini kwa nini
yaani!
Kuna kipi nisichokijua ina TV
ndani?
Usiulize n’takupa nini dada
piga moyo konde
Viuno vingi kama mwali wa
kimakonde
Usipende hela kama mfuko
Au fanya unavyofanya upate
zako
Vishawishi vingi binti sema
na moyo wako
Na ujifunze pesa zinauza utu
wako
Tajiri mtata kama Salah
Zipo ila sitoi me ni balaa
Unapenda hela zangu nami
nazipenda pia
Kila mtu abaki na zake bye
baby tutaongea
MWANAUME WA HIVYO WA NINI
SASA!!!!! Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii
tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema
Vanessa
Aje aje ajeeee me mtoto
fulani ghali
Nihonge gari Ma sweet sweet
baby
Wanna see you today unipeleke
party
Aje aje ajeee njoo nikupe TBT
MWANA FA
Siyo kwa enzi ya Magufuli
Zali ilikuwa long siku hizi
hakuna la mentali
Nikikuhonga na ukiniacha
nitakujia usingizini
Naepusha shari matatizo yote
ya nini
Hakuna kipya chini ya jua
Hata nisiyoyafanya
nishayasikia
Ningekuwa mhongaji
ningeshafulia wangu
Mademu wangu wa zamani wote
wangekuwa maadui zangu
MWANAUME HOVYO WEWE!!!!! Ndiyo
mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii
tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema
Vanessa
Baki na hamu zako
Kiitikio
VANESSA
Baba bure huyuu!!!
Mwana FA
Hata pantoni lina staff
Vanessa
Unamwambia nani sasa! Unamwaaambia
nani sasa!
Post a Comment