AZAM RASMI YATANGAZA, HAITASAJILI MCHEZAJI WA YANGA AU SIMBA, WAGENI WABAKIZA NAFASI MOJ
Uongozi wa Azam FC umebakiza usajili wa wachezaji watatu tu katika dirisha dogo.
Wachezaji
wawili watakuwa ni hapa nyumbani na mmoja kutoka nje ya nchi lakini
imeapa, kamwe haitasajili mchezaji kutoka Yanga au Simba.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba Byemba amesema wamekubaliana, Simba na Yanga, waendelee na mambo yao.
"Kweli
hili tumekubaliana wenzetu waendelee na yao na sisi tufanye yetu.
Tunaendelea na kufanya taratibu kupitia katika njia yetu.
"Tumebakiza nafasi moja ya mchezaji kutoka nje, pia tunataka wachezaji wawili kutoka hapa," alisema Kawemba.
Tayari
Azam FC imeanza masuala ya usajili kwa kusajili wachezaji kutoka nje ya
Tanzania. Imesajili washambuliaji wawili kutoka Ghana.
Kikosi
cha Azam FC chini ya Mhispania Zeben Hernandez hakikuwa na mwanzo mzuri
mwanzoni mwa Ligi Kuu Bara lakini kikaanza kubadili mwendo mwishoni
mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.

Post a Comment