1.
Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa
Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.
2.
Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha
Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.
3.
Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au
duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea
masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba
zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda
akaahirisha mwaka wake wa masomo.
4. Tunawasihi watanzania
kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya "Character
assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji
masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na
ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.
Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.
Ahsanteni.
Charles William Kaimu Ofisa Habari wake. 0716719589 (wilflow101@gmail.com). CnP
Post a Comment