Kwenye ‘Mpunga’ Trump si Mtu wa Mchezo Mchezo! Tazama Hapa Mijengo anayomiliki Dubai na Marekani
Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald John Trump.
Trump Ocean Club International Hotel.
Trump International Beach Resort
Ndege ya Donald Trump Boeing 757, yenye thamani ya dola millioni 100.
Donald Trump Tower amewekeza dola milioni 400, Dubai.
Trump Ocean Club International Hotel, ipo katika Jiji la Panama.
Jengo la Trump Hotel Las Vegas
Trump International Hotel & Tower Dubai
Trump Tower, Manhattan.
DONALD TRUMP JOHN alizaliwa 14
Juni 1946 huko Jamaica Estates, Queens akiwa ni mtoto wa pipi kwenye
familia ya watoto wanne wa familia ya Mary na Fred Trump na kukulia
katika Jiji la New York, Marekani.
Upande wa baba yake (Fred Trump
aliyefariki mwaka 1981), alikuwa mzaliwa wa Ujerumani na mama yake
(Mary) ni mzaliwa wa Scottish.
Trump alianza kusoma katika Chuo Kikuu
cha Fordham kilichopo Bronx mwaka 1964, miaka miwili baadaye
alihamishiwa katika Shule ya mambo ya fedha na Uchumi ya Wharton iliyopo
Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambako alihitimu shahada ya kwanza katika
masuala ya uchumi mwaka 1968 kabla ya kujiunga na kufanya kazi kwenye
kampuni ya familia yake iliyoitwa Elizabeth Trump & Son.
Mwaka 1971 Trump alikabidhiwa kuongoza
makampuni na biashara za baba yake ambapo alipata mafanikio makubwa
ndani ya muda mfupi ambayo mpaka sasa ndiye mkurugenzi wake mkuu.
Trump ambaye ni baba wa watoto watano,
ni mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchini Marekani, pia ni
mtayarishaji wa vipindi vya televisheni.
Baadhi ya mali anazomiliki
Trump Ocean Club International Hotel and Tower lililopo Panama City, Panama
Trump Tower lililopo Manhattan
Wollman Rink lililoko Central Park
Trump Taj Mahal lililoko Atlantic City, New Jersey
Turnberry Hotel, iliyoko Ayrshire, Scotland
Trump Hotel Las Vegas
Trump International Hotel & Tower ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Chicago
Trump International Hotel ya Las Vegas
Trump International Hotel ya Waikiki Beach Walk
Trump SoHo ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Toronto
Taasisi ya Donald J. Trump
Branding na licensing
Ndege kubwa ya Trump’s Boeing 757, maarufu kama “Trump Force One”.
Utajiri
Mwaka huu (2016), Jarida maarufu la
Forbes lilikadiria utajiri wa mali za Trump kuwa unafikia dola bilioni
3.7. Ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa mwenye utajiri mkubwa zaidi
kwenye historia ya nchi hiyo.
Ikijumulishwa na thamani ya kampuni yake
(brand), Trump anakadiliwa kuwa na utajiri sasa wa dola bilioni 10 na
kuwa tajiri namba 324 wa dunia na wa 156 kwa nchi ya Marekani.
Trump ni Mwenyekiti na Rais wa Shirika
Kibiashara la Trump (Trump Organization) lenye makao yake makuu katikati
ya Mji wa Manhattan ambalo linamiliki majengo mengi marefu, hoteli,
kasino, timu za gofu, ndege na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo
nchini Marekani na nje ya Marekani.
Ni mwanasiasa wa Chama cha Republican na
anagombea urais wa Marekani kupitia chama hicho mwaka huu, uchaguzi
utaofanyika Novemba 8.
Post a Comment