JERRY MURO AVUNJA UKIMYA, AIBUKA KIVINGINE NA KUZUNGUMZIA UKODISHWAJI WA YANGA

MTAZAMO WANGU
Nimesoma
hoja za wadau tangu juzi na jana, nimeona na kujifunza mengi sana
kutoka kwa waliokuwa viongozi wa yanga na wadau wa yanga kuwepo kwa
tofauti ya mitazamo ni jambo la afya katika uhai na maendeleo ya Yanga
hilo kwanza lazima tukubaliane.
Nichangie
kidogo hapa mimi kama Jerry muro nachangia kama mdau wa kawaida tu kwa
tulipofika sasa lazima tukiri kuwa tunaitaji club iongozwe na watu wenye
mitaji mikubwa ya fedha iwe kwa kukodishwa au kuwekeza mana mfumo wa
uendeshaji wa mpira duniani kote umebadilika kasoro Tanzania ambapo bado
tuko kama vile kwenye soka la ridhaa wakati mfumo unaotawala ni soka la
kimataifa na la kisasa.
Vilabu vya Tanzania vimekuwa kama vile ni vijiwe vya kufurahishana tu baada ya kazi na haswa kwa simba na y
Yanga
vikishafungana vyenyewe kwa vyenyewe biashara imekwisha hakuna
kifuatacho, na ndio mana tunapokwenda kwenye michuano ya kimataifa
tunapata shida mana sisi mtazamo wetu ni yanga amfunge simba basi mtaani
tushikishane adabu kwisha kazi.
Sasa tunachotakiwa ni kutoka hapa tulipo na kwenda mbele zaidi kwa kuwa na mfumo na muundo thabiti wa kimataifa.
Kwa
Yanga tumeanza na tunashukuru Mungu tumeanzia pazuri kwa kuwa sasa
muamko umekuwa mkubwa na umejenga mijada mingi sana ya kuonyesha dira ya
tuendako, hilo kwangu mimi ni afya kubwa sana kwa maendeleo ya Klabu.
Tusiwabeze
waliothubutu tuwasaidie kwa kuwaonyesha njia na kuwatia moyo mana
tukumbuke kila jambo Kiowa linaloanza kwa mara ya kwanza lina changamoto
kubwa zipo nyingine zinaweza kutatulika kwa sasa na haswa kwenye
mikataba na yako mengine yatakuwa yanajitatua taratibu yenyewe wakati
mfumo na muundo unaendelea cha msingi ni kuwa na SUBIRA.
Mwisho
nimalize kwa kusema kuwa hizi ni zama mpya zenye maono mapya na mwamko
mpya lazima tukubali kubadilika la sivyo tutabadilishwa kwa
lazima(nature will change us)
Kwa
wale wenye nia pia ya kusaidia yanga bado fursa zipo nyingi sana katika
maeneo mengine makubwa mfano mali za yanga majengo, kuwekeza kwenye
rasilimali watu ambao ni wanachama na mambo mengine, na tukiona hatuwezi
uko basi tuvute subira tusubiri baada ya miaka 10 tujitokeze
kuchangamkia fursa kutoka Yanga.
Niseme
kutoka moyoni kabisa Yanga ni yetu sote tusaidiane kuijenga yanga na
sio kuibomoa na katika yote lazima tukubali kuvumiliana katika madhaifu
yetu hakuna mkamilifu chini ya mbingu na jua hivyo KUVUMILIANA NI JAMBO LA BUSARA SANA.
Jerry Cornel Muro
Mdau wa soka Yanga
Post a Comment