YANGA MAMBO SAFI, SASA RUKSA KUTUMIA UWANJA WA UHURU
Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea keshokutwa
Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo kati ya Young
Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa
kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 6 kipendelea cha kwanza, Young Africans
wametambulisha Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa nyumbani kwa sasa baada ya
kuleta maombi Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) ambako baada ya
kuyafanyia tathimini kwa mujibu kanuni hiyo ya sita, kipendelea cha
sita, TFF imeiridhia klabu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, kutumia uwanja wa
Uhuru.
Hatua
hiyo inafuatia na Serikali – mmiliki wa viwanja vya Uhuru na Uwanja
Mkuu wa Taifa, kuzuia klabu hiyo pamoja na ya Simba kutumia Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kwa michezo yao ya nyumbani kutokana na vurugu.
Michezo
mingine itakayopigwa Jumatano ni kati ya Mbeya City ya Mbeya na Simba
ya Dar es Salaam, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya; Majimaji itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji
mjini Songea wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye
Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Stand
United itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini
Shinyanga na katika mkoa huo huo Mwadui itakuwa mwenyeji wa African Lyon
kwenye dimba la Mwadui Complex huku timu pinzani za Mwanza ‘Mwanza
Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans itapigwa Uwanja wa CCM Kirumba
jijini humo. Alhamisi Oktoba 13, 2016 Ruvu Shooting itacheza na Ndanda
FC kwenye Uwanja wa Mabatini.
Post a Comment