HATIMAYE MANCINI AFUNGUKA KISA KILICHOSABABISHA AMKWIDE BALOTELLI WAKATI WAKIWA MAN CITY
Hatimaye
Kocha Roberto Mancini amesema sababu iliyochangia kumkwida Mario
Balotelli wakati wote wakiwa wafanyakazi wa Manchester City ya England
mwaka 2013.
Picha zilizagaa mitandaoni wakiwa wanavutana huku Mancini raia wa Italia akionekana kuwa na jazba.
Lakini katika mahojiano na gazeti moja la Ufaransa, Mancini amesema alikasirishwa na tabia ya Balotelli ya kutosikiliza.
“Niliwaambia wachezaji wote, wawe makini na wenzao ambao walikuwa ni wagonjwa, wacheze kwa uangalifu.
“Mfano Gael
Clichy alikuwa ndiyo ametoka kwenye majeruhi. Nilisisitiza, lakini
ajabu Balotelli hakusikia, akamrukia. Nilikasirishwa sana kwa kweli,”
alisema.
“Lakini
kuhusiana na picha zile, hakukuwa na mvutano mkubwa sana kama
ilivyozagaa. Nilimvuta, nikataka kumuangusha lakini alikuwa imara sana
kuliko mimi, sikuweza. Lakini kweli nilikasirika sana.”
Post a Comment