MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZIA KESHO ZIKO HIVI...
Ligi
Kuu Bara inatarajiwa kuendelea leo Jumamosi kwa michezo mitatu ambako
Simba inayoongoza katika msimamo wa kuwania taji hilo katika timu 16
itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar
es Salaam.
Katika
mchezo huo Na.73, mwamuzi atakuwa Hussein Athuman kutoka mkoani Katavi
ambako pembeni atasaidiwa na Joseph Bulali wa Tanga na Silvester Mwanga
wa mkoani Kilimanjaro wakati Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi
wa akiba huku Kamishna wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.
Mchezo
mwingine utakuwa ni kati ya JKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga. Ni mchezo
Na. 74 utakaofayika Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani
ambako utachezeshwa na Mwanamama mwamzi mwenye beji la FIFA, Mwanahamisi
Matiku wa Dar es Salaam, akisaidiwa na Shafii Mohamed pia wa Dar es
Salaam na Gesper Ketto wa Arusha.
Mwamuzi wa akiba atakuwa Abdallah Rashid wa Pwani wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Charles Mchau wa Kilimanjaro.
Pia
Stand United ya Shinyanya itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa
CCM Kambarage katika mchezo Na. 75 ambao utachezeshwa na Eric Onoka wa
Arusha akisaidiwa na Agnes Pantaleo pia wa Arusha na Omary Juma wa
Dodoma wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Joseph Pombe wa Shinyanga.
Kamishna wa mchezo atakuwa Hamisi Kitila wa Singida.
Ligi
hiyo itaendelea keshokutwa Jumapili kwa mchezo utakaozikutanisha timu
za Azam na Young Africans; zote za Dar es Salaam. Mwamuzi wa mchezo huo
Na. 76 atakuwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo atasaidiwa na Soud
Lila na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote
wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar
es Salaam.
Mchezo
Na. 77 utazikutanisha timu za Ruvu Shooting na Mbeya City Jumapili
Oktoba 16, 2016 kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Mwamuzi wa
mchezo huo atakuwa Rudovic Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu
wa Arusha na Jeremina Simon wa Dar es Salaam. Kamisha wa mchezo huo
atakuwa Idelfonce Magali wa Morogoro.
Mtibwa
Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza Jumapili
Oktoba 16 kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. Mchezo huo Na. 78
utachezeshwa na Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi ni
Ferdinand Chacha wa Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa
akiba Nicolaus Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa
Dodoma.
Kwa
siku ya Jumapili mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Toto African ya
Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mchezo huo Na.
79 utachezeshwa na mwamuzi Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah
Uhako wa Arusha na Julius Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba
akiwa Mathew Akrama wa Mwanza. Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar
es Salaam.
Post a Comment