LIEWIG ATIBUANA NA STAND UNITED, AONDOKA AICHA TIMU KWENYE MATAA
LIEWIG |
Uongozi wa klabu ya Stand United umeingia kwenye mgogoro mkubwa na kocha wake, Patrick Liewig ambaye ameamua kuondoka kikosini.
Liewig
ameondoka katika kikosi cha Stand United kwa madai kwamba anadai
mshahara wake wa miezi miwili na amekuwa akilipwa zaidi ya dola 5,000
(zaidi ya Sh milioni 11) kwa mwezi.
Imeelezwa
baada wadhamini Acacia kujitoa kudhamini kutokana na mgogoro
ulioanzishwa na wenye hamu ya kuipata Stand United, imekuwa kazi kubwa
kumlipa kocha huyo.
Msemaji wa Stand United, Deo Makomba amethibitisha kuhusiana na Liewig kuondoka bila ya taarifa, lakini akasema wameshangazwa.
“Kocha
anajua kila kitu, tulimueleza hali yetu kutokana na suala la wadhamini.
Kwamba hatuko vizuri na baada ya miezi miwili tungemlipa.
“Lakini
sasa ameondoka hotelini, tunamtafuta hatujui yuwapi! Tena kuna watu
wanasema yuko Dar es Salaam, hili ni jambo linatushangaza sana.”
Kocha
huyo ameifanya Stand United kuwa moto wa kuotea mbali msimu huu kwani
baada ya mechi 9 ilizocheza, sasa iko katika nafasi ya pili kwenye
msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Post a Comment