Bia Ya Kopo Ya Safari Lager 500ml Yaendelea Kubamba Kitaa
Bila
shaka umeshaliona tangazo hili matata kabisa la Safari Lager ukipita
Barabara ya Kawawa jijini Dar, wajanja wanakwambia utaalamu uliotumia
kutengeneza bango hilo la 3D ni wa hali ya juu sana.
Tangazo hili limekuwa likiwavutia wapita njia katika barabarani hiyo na kuwateka hisia zao, “Dah yaani hili tangazo tu lilivyo linakufanya uitafute bia yenyewe uishushe kinywani” alisikika mmoja wa muenda kwa miguu.
Sasa
si tu kwamba tangazo linateka hisia na kuwa kivutio, bia yenyewe ina
ladha nzuri ya aina yake na inaleta urahisi na unafuu kwa mtumiaji
yeyote wa Safari Lager. Kampuni ya Bia ya TBL ilizindua bia hii ya kopo
ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania mwishoni mwa
mwezi wa 8 mwaka huu na hadi sasa imeonekana kuwa kipenzi cha watumiaji
katika maeneo mbalimbali nchini.
“Bia
mpya ya kopo ya Safari ni dhahiri kwamba imetengezwa kumpa umahiri
Mtanzania katika safari ya maisha yake. Inapatikana kwa urahisi na kwa
wakati muafaka hata wakati mtu anakwenda kwenye mihangaiko yake au
kubeba akiwa anakwenda kwenye matembezi au safarini” alisema Meneja
Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa
Meneja
Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa alipokuwa akitambulisha bia mpya ya
Safari Lager kwenye kopo la mililita 500 ambayo inapatikana Tanzania
nzima.
Baadhi ya wateja wakiwa na nyuso za furaha baada ya kujipatia bia mpya ya Safari Lager katika kopo lenye ujazo wa 500ml
Post a Comment