Hili la Kusagana, Mastaa Mnapaswa Kulikemea
Malkia Said a.k.a Malkies, binti wa miaka 19 aliyefunguka kuwa ni msagaji.
KWENU mastaa wa kike Bongo, nawasalimu kwa umoja wenu maana mpo wengi, siwezi kuwataja mmojammoja kwa majina.
Habarini za siku, vipi mnaendeleaje na
mishemishe za kila siku? Maisha yanasemaje? Hongereni kwa kuwa mastaa,
maana najua wapo wengi ambao wanatamani kuwa, lakini kwa namna moja au
nyingine wameshindwa.
Mkitaka kujua afya yangu, mimi ndugu
yenu sijambo. Namshukuru Mungu, naendelea kupambana katika eneo langu la
kazi. Nawahabarisha na kuwaelimisha Watanzania kupitia magazeti Pendwa
Bongo.
Nimewakumbuka leo mastaa wa kike kupitia
barua nzito, nina jambo nataka kuwaeleza na tafadhali sana,
lichukulieni suala hili kwa uzito wake.
Ndugu zangu, kwa muda mrefu nimekuwa
nikielezwa suala la mastaa kusagana. Tetesi zimewataja mastaa wengi tu
wa kike kwamba wanahusika katika mchezo huo. Najua mnajijua, sina sababu
ya kutaja majina yenu.
Nililifanyia kazi tetesi hizo na kubaini
kwamba zina asilimia nyingi ya ukweli ndani yake. Sababu kubwa
iliyotajwa kusababisha wengi wenu muingie kwenye mapenzi hayo ya jinsia
moja ni kutotaka usumbufu.
Kwamba wanaume wana usumbufu.
Wanawatumia kwa wakati fulani kisha wanawamwaga. Sababu nyingine
iliyotajwa ni kwamba mnafanya mchezo huo kwa sababu unawaepusha na
magonjwa hatari kama Ukimwi na mengineyo.
Kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele,
tatizo hilo linatajwa kushika kasi Bongo. Awali ilikuwa ni jambo la aibu
na siri, lakini siku hizi linafanyika bila hofu.
Naambiwa kwamba wahusika mnawajua. Kuna
wanawake ambao ndiYo mnawaita wanaume. Hivyo staa anaweza kuwa wa kike
lakini anawashughulikia wenzake au staa anaweza kuwa anashughulikiwa na
mwanamke mwingine ambaye anajifanya mwanaume.
Wiki iliyopita kupitia gazeti ‘dugu’ na
hili la Risasi Jumamosi, tuliona mrembo aliyejitambulisha kwa jina la
Malkia, akielezea kwa kirefu uzito wa tatizo hili. Akaenda mbali kwa
kusema alikuwa amnase mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ lakini ikashindikana
licha ya kuwa tayari alishamrushia ‘ndoano’ za kutosha.
Ndugu zangu hapa inatupasa kidogo
tumuogope Mungu. Hili ni tatizo, hakuna sababu ya kulifumbia macho.
Mnaofanya hivyo mjue kwamba huu si utamaduni wetu. Mambo hayo yamekuwa
yakifanywa huko ughaibuni.
Sidhani kama una manufaa kwetu. Sanasana
tunaharibu maadili na kizazi kijacho. Wanaoshiriki wabadilike, wafuate
utaratibu wa halali ambao ndio unafahamika hata katika maandiko ya dini.
Kwamba mwanaume atatembea na mwanamke na
wawili hao watapata mtoto. Uhusiano wa mwanamke kwa mwanamke tunautoa
wapi? Una faida gani katika jamii yetu?
Ni vyema tukachagua, kuishi katika
maadili yetu ya Kitanzania. Tukaachana na masuala ya kuiga ambayo
hayaleti picha nzuri katika jamii inayotuzunguka.
Wote mnaofanya vitendo hivyo mnajijua,
kila mmoja achukue hatua. Aache kabisa tabia hiyo kwani hata sababu
zinazowafanya muingie huko hazina mashiko, mnajidhalilisha.
Ni matumaini yangu mtakuwa mmenielewa na mtabadilika kitabia.
Mimi ni kaka yenu;

Post a Comment