Binti miaka 19 afunguka kuwa ni msagaji, ametembea na wake za watu 20 (Video zipo hapa na picha)
Malkia Said a.k.a Malkies.
Dunia Imekwisha!
Mayasa Mariwata na Hamida Hassan, Risasi Jumamosi
Dar: Dunia imekwisha! Ndiyo sentensi pekee inayoweza kukutoka baada ya kusikia kisa cha binti huyu aliyejitambulisha kwa jina la Malkia Said a.k.a Malkies, mwenye umri wa miaka 19, mkazi wa Magomeni jijini Dar ambaye amekiri kujihusisha na vitendo haramu vya usagaji akieleza alivyotembea na wanawake wenzake wasiopungua 40 wakiwemo wake za watu zaidi ya 20 hadi kufikia hatua ya kufumaniwa na kunyolewa nywele.
KABLA YA KUFUNGUKA
Kabla ya kufunguka yote hayo, awali
habari zake zilivuma kutoka pande mbalimbali jijini Dar na kwenye
mitandao ya kijamii ikidaiwa kwamba, mrembo huyo ni hatari kwa wake za
watu hivyo wenye ndoa zao wakae chonjo.
Baada ya kuvuma kwa jina hilo la Malkies
na sifa zake tajwa hapo juu huku ikidaiwa kuwa alifumaniwa na mke wa
mtu ndipo gazeti hili likajipa kibarua cha kumtafuta binti huyo ili
kujua mbivu na mbichi za msichana huyo.
HUYU HAPA MALKIES
Akizungumza na waandishi wetu ndani ya
ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar, mapema wiki hii, huku akiwa
macho makavu, Malkies alisema kuwa, alianza mchezo huo tangu akiwa mdogo
kutokana na hisia za mapenzi zilizokuwa zikimsukuma kwa kasi
kujihusisha na kitendo hicho haramu.
“Nilipokuwa mdogo, kuna binamu yangu
mara kwa mara alikuwa akinivizia akitaka kunibaka lakini nikawa
ninamchenga, sasa baba yangu alipofariki dunia nikiwa darasa la nne
ndipo nikapelekwa shule moja ya boarding iliyopo jijini Mwanza.
“Muda mwingi nilikuwa na watoto wa kike wenzangu huku msukumo wa kufanya nao mapenzi ukinitesa.
“Kwa kuwa yule binamu yangu alisababisha
niwe na hisia kali za mapenzi, nikawa navumilia. Mwisho, nilihamishiwa
shule nyingine ya boarding ipo Kibaha (Pwani).
“Huko kuna siku nikawa naumwa, rafiki
yangu Mzanzibari akataka kunichumu shavuni. Ndipo tukajikuta tumeingia
kwenye mchezo huo rasmi. Nakumbuka hiyo ilikuwa mwaka 2010,” alisimulia
Malkies huku akilengwalengwa na machozi.
ASHTUKIWA SHULENI
Alisema, baada ya hapo ilifikia hatua
uongozi wa shule ukajua na kuwaambia ndugu zake, akiwemo mama yake
lakini walipuuza kwa kuhisi anasingiziwa.
Alisema kadiri siku zilivyosonga ndivyo
alivyokubuhu na kupata uraibu uliomfanya kutotamani kuuacha mchezo huo
ambao aliamini ndiyo furaha pekee kwake kwani baada ya muda, mama yake
naye alifariki dunia.
AJARIBU KUWA NA WANAUME
Alidai kuwa, kutokana na maneno ya kila
kukicha watu wakimkemea juu ya ishu hiyo, Malkies aliona bora ajaribu
kuwa na mwanaume labda anaweza kuacha, lakini kila mwanaume aliyekuwa
naye ambao wanaweza kufikia ishirini, hakuwa akihisi msisimko kama
anapokuwa na wanawake wenzake.
“Pia mjomba wangu alikuwa akinikuta na
wanaume, ananipiga kwa sababu aliona umri wangu hauruhusu na hakujua kwa
nini nafanya hivyo maana nilishindwa kumwambia,” alisema Malkies mwenye
umri mdogo lakini aliyepitia mambo mengi ya kikubwa.
AFUMANIWA
Akiendelea kusimulia, Malkies alisema,
kwa kuwa anajitambua na anajua nini anachokifanya, alidhani ni vyema
kutoka na watu waliomzidi umri kuliko kuwapotosha vijana wa rika lake,
ndipo akampata mke wa mtu.
Alisema kabla ya hapo alishakuwa na wake
wengine wa watu lakini huyo wa Magomeni hali ilikuwa mbaya kiasi cha
kutwangwa talaka na mumewe.
“Nimeshakuwa na wake za watu zaidi ya
ishirini, wengi wamenizidi umri pia wake za watu wananitaka wenyewe,
huyo mmoja alikuwa anaishi Magomeni na mumewe akawa ananishumbua kwa
kipindi kirefu wakati mimi nilikuwa na mtu wangu.
“Nakumbuka ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu, nilipoachana na huyo mtu wangu (mwanamke mwenzake), niliamua kuwa na huyo mwanamke.
“Yeye ana umri wa miaka 30,
alinidanganya anaishi na baba yake, akanipeleka hadi kwake. Baadaye
aliniweka wazi kuwa anakaa na mumewe na majirani wakamfikishia habari
mume wake kuwa huwa nakwenda pale akiwa hayupo.
“Kulitokea ugomvi mkubwa kati ya yule mwanamke na mumewe, yule mwanamke akadai talaka na akapewa kwa sababu yangu.
“Niliendelea naye hata baada ya mumewe
kumuacha, tukawa tunaishi wote Ubungo kwa dada yake na mimi nikiwa na
mtu najiachia kimahaba siwezi kuficha.
“Wiki mbili baadaye, yule dada’ke alichukia, akaita ndugu zake na yule mume, wakaja kunifumania, wakanipiga na kuninyoa nywele.
“Tuliendelea kidogo lakini sasa
tumeachana kabisa,” aliongeza binti huyo ambaye pia aliwahi kushiriki
kwenye filamu na muziki japokuwa hakuwika.
STAA ANAYEMZIMIKIA
Akiendelea kueleza kwa kujiamini,
Malkies alisema, wanawake wengi ambao alikuwa akiwazimia ni Wazungu na
chotara, lakini mbali na hao alikuwa akiumiza kichwa na staa wa filamu
za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kumtunza Sh. milioni moja
kwenye shoo huko Arusha.
“Hakuna msanii anayenivutia zaidi ya
Wema na siku ile nilipomtunza ni kwa sababu tu alikuwa amelewa na mimi
nililewa, lakini tungekuwa sawa ningemueleza jinsi ninavyomkubali,”
alisema.
LENGO LA KUJITANGAZA
Alimalizia kuwa, suala hilo siyo jambo
la kufumbia macho kwa sababu linafanywa na wanawake wengi wakiwemo
mastaa na wake za watu hivyo ameamua kuanzisha shirika la kuwasaidia
wengine ambao bado hawajajiingiza na waliojiingiza kwenye vitendo hivyo
ili waache kwa lengo la kuokoa kizazi hiki na kijacho.
CHANZO: GPL

Post a Comment